Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Watuhumiwa 106 jela kwa uhalifu Arusha
Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa 106 jela kwa uhalifu Arusha

Spread the love

JESHI la Polisi mkoani Arusha limedai kuwa kuanzia Januari hadi Juni mwaka huu 2023 limewafikisha mahakamani watuhumiwa wa makosa makubwa ya uhalifu ambapo 106 walipatikana na hatia na kuhukumiwa kwenda jela vifungo mbalimbali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 21 Julai 2023 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo amesema watuhumiwa hao walihukumiwa vifungo hivyo kwa makosa makubwa ikiwemo ubakaji, ulawiti, kusafirisha dawa za kulevya, unyang’anyi wa kutumia silaha, mauaji pamoja na kupatikana na nyara za Serikali.

Kamanda Masejo amefafanua kuwa kati ya waliohukumiwa, watuhumiwa 25 walihukumiwa vifungo vya maisha jela kwa makosa ya ubakaji, ulawiti na mauaji.

Pia watuhumiwa 30 walihukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa makosa ya unyang’anyi wa kutumia silaha, kusafirisha dawa za kulevya, ubakaji na ulawiti huku wengine watano walihukumiwa vifungo vya miaka 20 kwa makosa ya kupatikana nyara za Serikali.

Mbali na hayo ACP Masejo amesema kuwa Jeshi hilo limepunguza matukio ya uhalifu mkoani humo kwa asilimia 11.

Amesema takwimu zinaonyesha kwa mwezi Januari hadi Juni 2022 makosa yalikuwa 1,345 hali ambayo ni tofauti na kipindi kama hicho mwaka huu ambapo makosa yaliyoripotiwa ni 1,198 sawa na upungufu wa makosa 147.

“Kwa kipindi kama hicho tumepunguza ajali za barabarani kwa asilimia 59 ambapo mwaka 2022 ajali zilizoripotiwa zilikuwa 184 ukilinganisha na ajali 76 zilizotokea mwaka huu ambapo ni sawa na upungufu wa ajali 108,” amesema.

Aidha, amesema kupitia misako mbalimbali ambayo ilifanyika kuanzia mwezi Januari hadi Juni mwaka huu dhidi ya dawa za kulevya walikamata mirungi kilogramu 747 na gramu 695, bhangi tani mbili na nusu pamoja na kuteketeza jumla ya tani tano na hekari 60 za bhangi lakini pia walikamata Heroine gramu 560.75.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!