Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto, Lipumba ‘waukwepa’ mkutano wa Dk. Slaa, Chadema
Habari za SiasaTangulizi

Zitto, Lipumba ‘waukwepa’ mkutano wa Dk. Slaa, Chadema

Prof Lipumba, Zitto
Spread the love

VIONGOZI machachari wa vyama vya upinzani, Profesa Ibrahim Lipumba (Mwenyekiti CUF) na Zitto Kabwe (Kiongozi Mkuu ACT Wazalendo) wametajwa kuutosa mkutano ulioandaliwa leo Jumapili Chadema kwa kushirikiana na Balozi mstaafu Dk. Wilbroad Slaa katika viwanja vya Bulyaga, Temeke, jijini Dar es Salaam.  Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Mkutano huo ulilenga kujadili kasoro zilizopo katika mkataba wa uwekezaji kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai katika bandari ya Dar es Salaam.

Licha ya wanasiasa hao kutarajiwa na wengi kushiriki katika mkutano huo hasa ikizingatiwa ni moja ya wanasiasa wa upinzani wanaokosoa mkataba huo, wanasiasa hao na wengine wa baadhi ya vyama vya siasa hawakushiriki.

Kutokana na hali hiyo, Kiongozi wa Sauti ya Watanzania, Dk. Slaa ambaye pia Katibu wa zamani wa Chadema, amesema katika dakika za mwisho za maandalizi ya mkutano huo, baadhi ya viongozi wa vyama vingine vya siasa wamejitoa kwa madai ya kuogopa vuguvugu hilo la Sauti ya Watanzania.

Bila kuwataja majina, Dk. Slaa amewataka viongozi hao wa siasa kuacha uoga kwa kuwa Sauti ya Watanzania inalenga kutetea rasilimali za Tanzania mahususi kwenye sakata la bandari.

Hata hivyo, katika mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya Bulyaga, Temeke, umeonesha wananchi wachache wamehudhuria mkutano huo.

Licha ya kuwa Dk. Slaa kujiweka mbele kama muandaaji wa mkutano huo, mkutano huo ulitawaliwa na viongozi wa CHADEMA, huku ikiwekwa nembo ya chama hicho na picha kubwa ya Mbowe kwenye bango nyuma ya meza kuu.

Makada wa CHADEMA pia wamekuwa wakiupigia debe mkutano huo kupitia mitandao ya jamii kama mkutano wa chama chao.

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini ilitoa onyo kwa CHADEMA kabla ya mkutano kwa kuwataka Chadema na Slaa kusitisha mkutano huo hasa ikizingatiwa unawahusisha maaskofu kwenye mikutano yao ya siasa siyo sawa kwani ni ukiukwaji wa sheria za nchi ambazo zinakataza vyama vya siasa kutumia udini kufikia malengo yao.

Hata hivyo, CHADEMA wamepuuza onyo la Msajili wa Vyama vya Siasa na kuwapandisha maaskofu kwenye jukwaa katika mkutano wao wa leo wa Temeke, kinyume na sheria za nchi.

“Msajili anatuandikia barua anasema mnakwenda kuzungumza viongozi wa dini na taasisi nyingine. Aliyemuambia mkutano wa hadhara tunazungumza na wanaChadema peke yake ni nani?” amesema Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!