ALIYEKUWA Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia leo Jumapili ametoa wito kwa Serikali kuacha kiburi na kukubali kurudi kwenye meza ya mazungumzo ili kutafuta suluhu kuhusu mkanganyiko uliojitokeza katika mkataba unaohusu uwekezaji kwenye bandari ya Dar es salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).
Mbatia ametoa wito huo leo tarehe 23 Julai 2023 jijini Dar es Salaam katika mkutano ulioandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Balozi Dk. Willbroad Slaa na wenzie kwa lengo la kujadili kasoro zilizomo katika mkataba wa ushirikiano wa kiserikali kati ya Tanzania na Dubai, kuhusu uwekezaji wa bandari,
Amesema huu ni wakati wa sayansi na teknolojia hivyo ni vema ikubali kukaa na watalaam ili kutoka kwenye mtanzuko huo kwani Taifa likiangamia na wote wataangamia.
“Ikikubali kukaa kwenye meza ya mazungumzo hakuna kilicho siri, kwenye ulimwengu wa leo hakuna kilicho siri penda tusipende ukweli umewekwa wazi. Turudi pamoja kwenye ubora wa Taifa letu ili libaki kuwa salama… ukiona uovu unatendeka zuia, ukishindwa kuzuia kemea, ukishindwa onesha chuki,” amesema.
Mbatia amesema Taifa lipo katika janga, limegawanyika, linazama hivyo inahitaji hekima ya Mungu ili kurudisha Taifa pamoja.
“Tiba zipo za aina mbili… tutumie ibara ya nane ya katiba ambayo ni nguvu ya umma pili ni watu wenye dhamana kukaa pamoja ili kupata suluhu,” amesema.
Leave a comment