February 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Yondani kuikosa Singida United

Spread the love

BEKI wa Yanga, Kelvin Yondani ataukosa mchezo Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida United unaotarajia kuchezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baaada ya kuoneshwa kadi tatu za njano katika michezo mitatu iliyopita. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Nahodha huyo ambaye alioneshwa kadi mfululizo katika michezo dhidi ya Stand United, Coastal Union na Mtibwa Sugar hivyo kutokana na kanuni za ligi hiyo atakosa mchezo unaofuata.

Katika hatua nyingine uongozi wa klabu hiyo umetoa taarifa ya kuwasamehe wachezaji Haji Mwinyi, Pius Buswita, Said Makapu na Ramadhani Kabwili baada ya kuomba msamaha kwa uongozi pamoja na benchi la ufundi kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu.

Sababu za kabwili kuondolewa kwenye kikosi ni baada ya kuchelewa wakati wa kula timu ilipokuwa kambini, huku kwa upande wa wengine watatu walitakiwa kuwapo uwanjani wakati timu hiyo ilipokuwa ikiminyana na Stand United licha ya kutokuwa sehemu ya kikosi katika mchezo huo lakini waliamua kukaidi na kuingia mitini.

error: Content is protected !!