March 9, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Waliofariki MV Nyerere wafika 94

Spread the love

IDADI ya watu waliofariki dunia katika ajali ya kivuko cha MV. Nyerere katika Ziwa Victoria jana. Anaripoti Mwandishi Maalum … (endelea).

Mpaka kufika saa 4 leo asubuhi pekee wameopolewa maiti 50 ambapo jioni jumla ya maiti 44 waliopolewa.

Watu 40 wanaripotiwa kuokolewa wakiwa hai mpaka sasa na wanaendele na matibabu.

John Mongella, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza anasema, utafutaji wa miili mingine unaendelea.

Viongozi mbalimbali wapo eneo la tukio wakiendelea na harakati za uokoaji.

Miili ya maiti hao imehifadhiwa kwenye Kituo cha Afya cha Bwisya kwa mujibu wa Mongella.

Kivuko cha MV. Nyerere kilizama jana ziwani humo ikiwani kilomita 50 kabla ya kutia nanga kwenye Kisiwa cha Ukara ilipokuwa ikielekea.

Raila Odinga, Kiongozi wa upinzani wa muungano wa NASA nchini Kenya amemtumia salama za pole Rais wa Tanzania na Wananchi wote kutokana na ajali ya MV. nyerere.

“Naomboleza na raia wa Tanzania katika kipindi hiki kigumu. Mungu awape amani na utulivu…” ameandika Odinga katika ukurasa wake wa Facebook.

error: Content is protected !!