Monday , 4 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kuzama MV Nyerere: Lowassa, Mbatia, Maalim Seif wamvaa JPM
Habari za Siasa

Kuzama MV Nyerere: Lowassa, Mbatia, Maalim Seif wamvaa JPM

Spread the love

JAMES Mbatia, Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi-Taifa amesema, ajali ya MV. Nyerere iliyotokea jana katika Ziwa Victoria ni ya kujitakia. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Mbunge huyo ametoa kauli hiyo leo tarehe 21 Septemba mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Mbatia amebainisha kuwa kuzama kwa meli hiyo kulikuwa kumetabiriwa na kwamba, wahusika walikuwa wakijua.

Amesema kuwa, asilimia 96 ya majanga yanasababishwa na wanadamu na kuwa, asilimia nne tu ndio ya asili.

Amesema kuwa, Tanzania ingejifunza katika matukio kama hayo ambayo yaliwahi kutokea akitaja kuwa ni Spice Islander na ile ya MV Bukoba.

“Zile ajali zingetosha kuwa fundo na hata hizi nyingine zisingetokea,” amesema Mbatia na kwamba, ajali hizo zikitokea viongozi na watu wengine huishia kutoa pole ambayo haisaidii chochote.

Hata hivyo ameshauri kuanzisha kwa sheria ya wakala wa usimamizi wa maafa kwa lengo la kuwalinda na kuwakinga Wananchi.

Maalim Seif Shariff Hamad, Katibu Mkuu wa CUF ameeleza kukerwa na uamuzi wa kusitisha uokoaji jana jioni.

Kutokana na uzembe na kusababisha uokoaji kusimama, Maalim Seif ameshauri viongozi wa sekta hiyo pamoja na waziri wanapaswa kuwajibiki ikiwa ni pamoja na kujiuzulu.

Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu amesema kuwa, huu ni msiba wa kitaifa.

Ameshauri kuwa serikali na taifa vinapaswa kujipanga ili ajali za namna hii zisitokee tena.

Lowassa amesema amestushwa na ajali hiyo ambapo ametoa pole kwa wafiwa na kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwinyi aungana na Samia kuuaga mwili wa baba yake

Spread the loveRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk....

Habari za SiasaTangulizi

Mtoto wa Mzee Mwinyi amwaga machozi

Spread the loveMtoto wa Hayati mzee Mwinyi, Abdullah Ali Hassan Mwinyi ameshindwa...

Habari za SiasaTangulizi

Mzee mwinyi alikuwa mwanademokrasia wa kweli

Spread the loveMtoto wa Hayati Ali Hassan Mwinyi, Abdullah Ali Hassan Mwinyi...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Mwinyi alikuwa maktaba inayotembea

Spread the loveRais Samia Suluhu hassan amesema Hayati rais mstaafu, Ali Hassan...

error: Content is protected !!