Friday , 1 March 2024
Home Kitengo Michezo Yanga kucheza na Aigle Noir kilele siku ya Mwananchi
Michezo

Yanga kucheza na Aigle Noir kilele siku ya Mwananchi

Dk. Mshindo Msolla, Mwenyekiti wa Yanga
Spread the love

KLABU ya Yanga inatarajia kucheza na timu ya Aigle Noir kutoka Burundi katika kilele cha Tamasha la Siku ya Mwananchi, linalotarajiwa kufanyika Jumapili 30, Agosti kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Tamasha hilo ambalo linafanyika kwa mwaka wa pili, huku likiwa na lengo la kutambulisha wachezaji wapya pamoja na wazamani watakaotumika katika msimu mpya ujao wa mashindano.

Timu hiyo ambayo inatarajia kutua nchini hivi karibuni, imeshika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini Burundi katika msimu wa Ligi uliomalizika ikiwa na pointi 48.

Timu ya Aigle Noir ya Burundi

Mchezo huo ambao unaweza kutumika kama kipimo kwa Yanga katika maandalizi yake kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaotarajia kuanza 6 Agosti ambapo Yanga itashuka dimbani dhidi ya Tanzania Prison kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Yanga mpaka sasa imesajili jumla ya wachezaji 10 kutoka ndani na nje ya nchi huku ikiwa imeacha wachezaji 14, ambao walitumikia klabu hiyo katika msimu wa Ligi uliomalizika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Wizara yaahidi kuboresha, kuimarisha michezo

Spread the loveIkiwa ni saa kadhaa baada ya kumalizika kwa mashindano ya...

Habari MchanganyikoMichezo

Nje jogging yanyakua medali 20 Kili Marathon

Spread the loveTimu ya riadha ya Wizara ya Mambo ya Nje na...

Michezo

Siku ya kukusanya maokoto ni leo, usipange kukosa

Spread the love  HATIMAYE Jumamosi imefika ndugu mteja wa Meridianbet na mechi...

Michezo

Kuwa milionea na Meridianbet ni rahisi sana

Spread the love  JE, unajua kuwa leo hii ni siku nzuri kwako...

error: Content is protected !!