May 15, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Butiku awaonya wapinzani, wasimamizi wa uchaguzi

Spread the love

JOSEPH Butiku, Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, amevita vyama vya upinzani nchini Tanzania, kuacha kuipinga Serikali kwa kutumia maneno ya matusi na kejeli ikiwemo kumsema vibaya hadharani Rais John Pombe Magufuli. Anaripoti Faki Sosi …(endelea).

Pia, amevitaka vyombo vyote vinavyosimamia Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020, kuhakikisha vinatenda haki kwa kila mmoja ili Watanzania waweze kuchagua kwa uhuru na heshima viongozi wanaowataka.

Butiku ameyasema hayo leo Jumatatu tarehe 24 Agosti 2020 kwenye Kongamano la maombi na dua kwa ajili ya uchaguzi mkuu huo lililofanyika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Kongamano hilo lililoandaliwa na Kamati ya Maridhiano, limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini, kiserikali na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania.

Mwenyekiti wa NEC, Semistocles Kaijage

Akizungumza katika kongamano hilo, Butiku amesema, licha ya Rais Magufuli kufanya mambo mazuri lakini hawezi kukwepa kukosolewa kwa kuwa hawezi kumridhisha kila mtu.

“Na mimi napenda kwa niaba ya Taasisi kumpongea Rais wetu kwa kazi mzuri aliyoifanya, kama yapo mapungufu tukumbuke Mwalimu Nyerere alikiri akisema, ukiwa na madaraka ni vigumu kukwepa kutumia madakaraka kwa kiwango kisichoridhisha wengine.”

“Anaweza tu kusimamia mambo ya msingi na kwenye mambo ya msingi ameyasimamia kwa kiwango kikubwa maendeleo yetu,” amesema Butiku

Amesema, wapinzani waache kumpinga Rais Magufuli kwa kutumia lugha ya matusi.

“Tuwashauri namna ya kupinga, wasipinge kwa matusi tena wasitukane baba zoa, Rais ni baba yetu, wasitukane Rais ni jambo la hovyo, mnamdharirisha mbele ya watu, mbele ya watoto, wewe umazaliwa wapi unayetukana watu hovyo si mtoto mwema,” amesema Butiku

Pia, Butiku amekemea watu wanaotoa rushwa ili kupata uongozi akisema, “mtu wa aina hiyo ni ibilisi” na kuwataka viongozi wa dini kwenda kukemea vitendo hivyo na wale wenye mamlaka ya kusimamia uchaguzi watende haki.

“Wapeni nafasi Watanzania hawa wapige kura Bara na Visiwani kwa uhuru, niliwahi kusema na leo ngoja nirudie, ninyi woooote mnaoshiriki kuwezesha uchaguzu huu, kila mtu afanye wajibu wake, msiwaonee wananchi wa Tanzania.”

“Msiwanyang’anye uhuru wao, msiwanyany’anye nafasi yao, msitende vituko katika kutenda nafasi ya kwenda kupiga kura, uwe polisi, jeshi uwe nani, wapeni uhuru wapige kuru na kwa heshima,” amesema

“Na mambo yote tuliyokuwa tunatenda siku za nyuma yaishe kuanzia kikao hiki, watu wa dini mtusaidie, mtuombee, Mungu atutazame,” amesema Butiku.

Akitumia jukwaa hilo hilo akisema kuwa upinzani ni haki ya kila mtu ikiwemo kupinga na kuikosoa serikali lakini sio kwa kila jambo.

IGP Simon Sirro

“Kuwa mpinzani sio kupinga kila kitu, kumpinga Rais sawa na kumpinga baba yako, hivi mtoto wako akipiga kelele utamwacha aendelee kupiga kelele chumbani si unamfuata? vyama hivi vimepiga kelele, kelele hizo zimetufanya tumewakimbilia kidogo,” amesema

Butiku amesema, licha ya waasisi kuweka misingi imara lakini nchini imepita kwenye changamoto za kushindwa kusimamia rasilimali, viwanda, kushindwa kudhibiti rushwa na kwamba misingi hiyo imerejeshwa na Rais wa awamu ya tano, Magufuli.

“Tulishindwa kulipa kodi, miradi yetu mingi ilikufa, AirTanzania, reli zetu, umeme wetu, tumekaa gizani kwa miaka mingi, hata Strigle’s George tulishindwa, kuhamia hapa Dodoma lakini kwa sasa haya yote yamefanyika”, amesema Butiku.

Amesema mradi wa Striggle’s George ulishindwa kufanywa na viongozi waliopita kutokana na kikwazo kilichowekwa na Benki ya Dunia (WB) lakini Rais Magufuli ameruka kihunzi hicho na mradi huo umeanza.

Amesema, Rais Magufuli ametumia njia ya kipekee ya kiubunifu yenye uadilifu juu ya kueleza alama anaziweka nchini.

Amewasifu viongozi wa dini kwa kuanzisha utaratibu wa kumsifu Rais kwa utendaji wake na kwamba kitendo hicho kinatia moyo.

Butiku amesema, Rais Magufuli anastahili kusifiwa kwa kuweza kufanya mambo ambayo viongozi wengine waliopata kushika hatamu walishindwa kuyafanya

error: Content is protected !!