Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Wizara ya Elimu kuchunguza tuhuma vitendo vya ulawiti shuleni
Elimu

Wizara ya Elimu kuchunguza tuhuma vitendo vya ulawiti shuleni

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, imetuma timu maalum kwenda mkoani Kilimanjaro kuchunguza tuhuma za wanafunzi kufundishwa vitendo vya ulawiti katika baadhi ya shule mkoani humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Tuhuma hizo zimeripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Waziri mwenye dhaman ya Elimu, Prof.Adolf Mkenda amesema timu hiyo inaongozwa na Kamishna wa Elimu, Mwanasheria wa Wizara na Mkurugenzi wa Uthibiti Ubora.

“Tumeshtushwa sana na jambo hilo,tumelichukua suala hili kwa umuhimu mkubwa tumeongea na Mkuu wa Mkoa na kama kuna jinai yeyote basi hatua za kisheria zichukuliwa mara moja.” Amesema Waziri Mkenda.

Prof, Mkenda amesema kwamba timu hiyo imeshaanza ‘uchunguzi’ katika shule zilizotajwa na hatua za haraka zitachukuliwa kwa wahusika wote watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo.

Waziri wa Elimu, Prof.Adolf Mkenda

Waziri Mkenda ameongeza kuwa wizara ya Elimu itatoa namba maalumu ili kuwezesha wananchi kutoa taarifa za vitendo hivyo vinavyochafua taswira ya elimu, kuondoa imani ya wazazi kwa shule na kuharibu vijana ambao ndiyo nguvu kazi ya Taifa.

“Katibu Mkuu atatangaza namba ambayo mtu yeyote akijua kuna vitendo kama hivyo kwenye shule au chuo chote nasi tutaifanyia kazi kwa kufanya uchunguzi ili kudhibiti vitendo hivyo” ameeleza Prof.Mkenda.

Prof. Mkenda ameongeza kuwa katika kuweka mipango endelevu ya kudhibiti vitendo hivyo Wizara ya Elimu,Sayansi na teknolojia inashirikiana na wizara nyingine za kisekta katika kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsi katika jamii ikiwemo maeneo ya shule na vyuo nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari Mchanganyiko

Waliopata Division one St Anne Marie Academy waula, Waahidiwa kupelekwa Ngorongoro, Mikumi

Spread the love WANAFUNZI wa shule ya St Anne Marie Academy waliofanya...

ElimuMakala & Uchambuzi

Waraka maalumu kwa NECTA, “hawapaswi kuungwa mkono”

Spread the loveHATUA iliyotangazwa na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), ya...

Elimu

NACTVET yafungua dirisha la udahili

Spread the love  BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo...

Elimu

Prof. Mwakalila awafunda wanafunzi Chuo Mwalimu Nyerere, “ulipaji ada ni muhimu”

Spread the love  MKUU wa Chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere (MNMA),...

error: Content is protected !!