Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Likizo ya Mch. Kimaro: Waumini Kijitonyama waonyesha hisia zao
Habari MchanganyikoTangulizi

Likizo ya Mch. Kimaro: Waumini Kijitonyama waonyesha hisia zao

Spread the love

 

BAADHI ya waumini wa Kanisa la KKKT Usharika wa Kijitonyama jijini Dar es Salaam wamejitokeza mbele ya kanisa hilo wakiwa na mabango yenye jumbe mbalimbali za kupinga hatua ya viongozi wa juu wa kanisa hilo kumpa likizo ya siku 60 Mch. Dk. Eliona Kimaro aliyekuwa akihudumu katika usharika huo, kwasababu ambazo bado hazibainika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa ya likizo ya Mchungaji Kimaro, zilizoanza kuenea katika mitandao ya kijamii na zimezua hisia tofauti miongoni mwa waumini na wasio waumini wa kanisa hilo.

Leo jioni MwanaHALISI Online imefika kanisani hapo na kushuhudia kundi la waumini walioketi katika viti nje ya kanisa hilo wakiwa na mabango huku wakiimba nyimbo za kutia hamasa.

Pia imeshuhudiwa kudorora kwa mahudhurio ya watu katika Ibada ya jioni na hata ile ya asubuhi kwa mujibu wa mashuhuda tofauti na siku za nyuma.

Kupumzishwa kwa Mch. Kimaro kunaweza kusababisha mpasuko mkubwa katika kanisa hilo kutokana na ushawishi wake kuwa mkubwa kwa waumini wengi wa usahrika huo na hata nje ya usharika.

Kupumzishwa kwa Mchungaji huyo aliyejipatia umaarufu nchini kwa mafundisho ya aina yake, kumezua gumzo katika mitandao ya kijamii baada ya kusambaa kwa video inayomwonesha Kimaro akiwaaga waumini wake jana.

Kimaro alitangazia waumini katika video hiyo kuwa majukumu yake yatafanywa na Mchungaji Anna na kueleza kuwa barua hiyo ya likizo imemwelekza kuripoti makao makuu ya Dayosisi tarehe 17 Machi mwaka huu.

“Imenilazimu kutii na kwenda kwenye hiyo likizo ya siku 60 na baadae kuripoti katika ofisi ya askofu kama nilivyoelekezwa na ofisi ya askofu,” amesema Mch. Kimaro.

Katika andiko lake Askofu Mwamakula amesema huenda misimamo binafsi ya Mch. Kimaro ndiyo imemuweka katika misukosuko.

Kusimamishwa kwa Mch. Kimaro kumeibua wanasiasa na wanaharakati wengi kueleza hisia zao juu ya hatua hiyo ambapo aliyewahi kuwa Meya wa Ubungo Boniface Jacob ameandika katika ukurasa wake wa twitter, “binafsi sishangai kabisaaa kuona maelfu ya Watu wameguswa kuhusu sakata la Mch.Kimaro,

Mchungaji Kimaro amekuwa Msaada kwa Watu na familia nyingi sana KIMARO unamwambia “biashara zangu haziendi vizuri”akwambii tupige magotini tusali,bali mnaanza Kijadili ‘Principles’ za biashara.”

Naye James Mbowe ameandika, “hii taarifa imenistua sana usiku huu, mimi ni mlutheri nitaandika maoni yangu kesho, akili ikitulia.

Duru zinaeleza kuwa huenda kusimamishwa kwa Mch. Kimaro kuna husiana na kauli zake ambazo zimekuwa na utata.

Kwa mujibu wa video iliyosambaa, Mch. Dkt. Kimaro amesikika akisema kuwa vijana wa Kikristo sio waaminifu kama vijana wa Kiislamu pia amewahi kusikika katika video moja akisifu Kanisa Katoliki dhidi ya makanisa mengine.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga

Spread the love  MAJINA 12 kati ya 17 ya waliofariki dunia katika...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awalilia 17 waliofariki ajalini wakisafirisha maiti

Spread the love  RAIS Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa...

Habari Mchanganyiko

Wanawake wachimbaji wajenga zahanati kuokoa afya za wakazi 2000

Spread the love  ZAIDI wakazi 2,000 wa kijiji cha Nyamishiga Kata ya...

Habari Mchanganyiko

Baada ya Congo DR, Somalia mbioni kujiunga na EAC

Spread the love  TAIFA la Somalia liko mbioni kuwa mwanachama rasmi wa...

error: Content is protected !!