Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Waziri Ummy aagiza wakuu wa mikoa, wilaya kusimamia chanjo polio
Afya

Waziri Ummy aagiza wakuu wa mikoa, wilaya kusimamia chanjo polio

Ummy Mwalimu
Spread the love

 

WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu ameagiza wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya nchini kusimamia kikamilifu utekelezaji wa kampeni ya chanjo ya matone inayotolewa kwa watoto chini ya miaka mitano ili kuhakikisha watoto wote wamepatiwa huduma hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Ummy alisema chanjo matone ya polio ni chanjo inayotolewa siku zote katika ratiba ya kawaida ya chanjo katika vituo vya kutolea huduma za afya hapa nchini;

“Ninatoa wito kwa wakuu wa mikoa na wilaya zote nchini kusimamia kampeni hii ili kumfikia kila mtoto popote alipo kwa lengo la kuhakikisha kila mtoto anapata kinga na kuzuia ugonjwa huu usiingie nchini kwetu.

Kwa mujibu wa Ummy, kampeni hiyo iliyoanza kutekelezwa Machi 24 hadi 27, katika mikoa ya Songwe, Njombe na Ruvuma imeshirikisha pia wadau wa afya, Shirika la Afya Duniani (WHO); “Kampeni ililenga kuwafikia watoto 975,839 wenye umri chini ya miaka mitano na kufanikiwa kuwafikia watoto 1,130,261 sawa na asilimia 115 ya walengwa wote.

“Awamu ya pili ya kampeni hii ilifanyika nchi nzima Mei 18/21 ikiwa na malengo ya kuwafikia watoto 10,295,316 wenye umri chini ya miaka mitano na kufanikiwa kuwafikia watoto 12,131,049 sawa na asilimia 117.8 ya walengwa wote.

Ummy aliongeza kusema kwamba serikali inaelekea kutekeleza awamu ya tatu ya kampeni ya kutoa chanjo ya matone ya polio iliyoanza Septemba na itakuwa kwa nchi nzima; “Awamu hii ya tatu imelenga kuwafikia watoto 12,386,885 wenye umri chini ya miaka mitano.

Akizungumzia athari ya ugonjwa wa polio, Ummy alisema ni ugonjwa unaosababishwa na kirusi ambacho huambukizwa kutoka mtu aliyeathirika kwenda kwa mtu mwingine kwa kula au kunywa kitu kilichochafuliwa na kinyesi chenye virusi vya polio.

“Virusi hivi vinapoingia mwilini huathiri mfumo wa fahamu na kusababisha madhara ya kiafya ikiwa ni pamoja na kupooza kwa ghafla kwa viungo na kusababisha kifo. Dalili za awali za polio ni pamoja na homa, uchovu, maumivu ya kichwa, kutapika, kukamaa shingo na maumivu ya kichwa.

“Vilevile ugonjwa wa polio hauna tiba. Njia kuu ya kuzuia ugonjwa ni pamoja na kuwapatia chanjo watoto walio chini ya miaka mitano. Chanjo hizi zimekuwa zikitolewa kupitia vituo vya kutolea huduma za afya ya mkoba na kliniki tembezi.

Ummy amewaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa timu za wachanjaji watakapofika katika maeneo yao, kupita nyumba kwa nyumba na maeneo yote alipo mtoto wa chini ya miaka mitano.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

AfyaHabari Mchanganyiko

Songwe katika mikakati ya elimu ya lishe kudhibiti udumavu

Spread the love  SERIKALI mkoani Songwe imejipanga kuendelea kutoa elimu ya lishe...

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

error: Content is protected !!