Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bashungwa: Tozo ni mwarobaini maboresho ya sekta muhimu
Habari za Siasa

Bashungwa: Tozo ni mwarobaini maboresho ya sekta muhimu

Innocent Bashungwa
Spread the love

 

WAZIRI wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) nchini Tanzania, Innocent Bashungwa, amesema tozo za miamala zimekuwa mwarobaini wa kuboresha sekta muhimu za wananchi ambazo ni Elimu, Afya na miundombinu kati ya Januari 2020 hadi Desemba 2020. Anaripoti Felister Mwaipeta, TUDARCo … (endelea)

Amesema sekta ya afya ikiwa ni sekta muhimu kwa binadamu kati Januari hadi Desemba 2020, Serikali imejenga Hospitali 102 za wilaya pia, imejenga vituo 407 vya Afya pamoja na zahanati 1,198.

“Serikali haikuishia hapo katika suala la afya ndani ya mwaka mmoja kulijengwa vituo vya afya 207 kwa kuwa serikali ilibaini changamoto ya umbali wa takribani kilometa 60 kutoka Tarafa moja kwenda nyingine kupata huduma za afya,” amesema Bashungwa.

Waziri, Bashungwa, ameendelea kusema kupitia tozo za miamala Serikali ilikusanya kiasi cha Sh. 234 billioni na kufanya maboresho ya vituo mbalimbali vya afya zikiwemo hospitali na zahanati ambapo kila kituo cha afya kiligharimu millioni 500.

“Lakini tulipeleka vifaa tiba vya kisasa vilivyogharimu 149.5 billioni ambayo pia ilitumika katika ujenzi wa wodi ya kina mama na watoto, vifaa vya kisasa kama vile, utra sounds, CT Scan, vitanda pamoja na ujenzi wa majengo ya wafanyakazi ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wakati,” amesema.

Aidha, Waziri, huyo aliendelea kusema katika suala la Elimu ambalo ndo linabeba nguvu kazi ya nchi yetu kwa kuwa inatupatia wasomi alisema sera ya elimu bila ada kiasi cha shilingi 346.5 billioni kimetengwa ili kuwapunguzia gharama wazazi.

Amesema tozo zimechangia kujengwa kwa madarasa 15000 na kuhakikisha watoto wote wanapata nafasi ya kusoma bila taabu yoyote.

Aliendelea kwa kutoa tathimini iliyofanywa na serikali kupitia wizara ya Tamisemi kwa kusema tunatakiwa kujenga madarasa yasiyopungua 15000 kila mwaka ili kuboresha sekta ya elimu.

Aidha, amesema katika suala la Tarura, bajeti imeongezeka kutoka Sh 272.5 billioni hadi Sh 802.29 billioni kwa kila shillingi 100 ya kila lita ya petroli na dizeli inayotolewa na wananchi kupitia tozo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!