Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Waziri Uganda auawa na mlinzi wake
Kimataifa

Waziri Uganda auawa na mlinzi wake

Charles Okello Engola
Spread the love

 

MWANAJESHI wa Jeshi la Uganda amempiga risasi na kumuua waziri katika Serikali ya Uganda ambaye alikuwa akimlinda.

Kanali mstaafu Charles Okello Engola, ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Kazi, alipigwa risasi nyumbani kwake katika mji mkuu, Kampala leo Jumanne asubuhi. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa.

Haijajulikana wazi iwapo kulikuwa na mabishano kati yake na mkuu wake, kabla ya kumpiga risasi.

Baadhi ya mashahidi walisema askari huyo alizunguka kwenye maeneo jirani akifyatua risasi hewani.

Hatimaye mwanajeshi huyo, ambaye hajatambuliwa rasmi, alijipiga risasi na kufa dakika chache baadaye.

Taarifa zinasema kuwa watu kadhaa wamejeruhiwa katika tukio hilo.

Video kwenye mitandao ya kijamii inaonyesha wenyeji wa eneo hilo wakikusanyika katika eneo la tukio kwa mshituko.

Kanali Engola awali alihudumu kama Naibu Waziri wa Ulinzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

error: Content is protected !!