October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waziri Mkuu kuzindua kampasi ya CBE Mbeya Oktoba 8

Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Profesa Emmanuel Mjema, akizungumza na waandishi wa habari kutangaz kilele cha harambee ya kutafuta Sh bilioni 1.2 kuchangia ujenzi wa mabweni ya wasichana itakayofanyika Jumamosi hii jijini Mbeya. Kushoto ni Naibu Mkuu wa chuo, Mipango, Fedha na Utawala, Dk. Emmanuel Munishi na kulia ni Ofisa Uhusiano wa chuo, Leonidas Tibanga

Spread the love

 

CHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimesema mwitikio wa wadau mbalimbali kuchangia ujenzi wa mabweni ya wasichana katika kampasi yake mkoani Mbeya imekuwa ya kutia moyo. Na Mwandishi Wetu

Hayo yalisemwa jana chuoni hapo jijini Dar es Salaam, Profesa Emmanuel Mjema, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kilele cha harambee hiyo inayotarajiwa kufanyika Jumamosi hii jijini Mbeya.

“Tunashukuru mwitikio umekuwa mzuri na mkubwa watu wamejitoa kuendelea kuchangia na wengine wamethibitisha kwamba watakuja Mbeya kushiriki harambee hivyo tunawashukuru na kuwataka wengine waendelee kuchangia,” alisema

Vile vile, alisema (CBE), imekamilisha ujenzi wa kampasi yake mkoani Mbeya yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 2,000 na mpaka sasa kimeshachukua wanafunzi 1,000 tayari kwa kuanza masomo.

Alisema majengo ya chuo hicho yanatarajiwa kuzinduliwa Oktoba 8 mwaka huu jijini Mbeya na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Profesa Emmanuel Mjema, akizungumza na waandishi wa habari kutangaz kilele cha harambee ya kutafuta Sh bilioni 1.2 kuchangia ujenzi wa mabweni ya wasichana itakayofanyika Jumamosi hii jijini Mbeya. Kushoto ni Naibu Mkuu wa chuo, Mipango, Fedha na Utawala, Dk. Emmanuel Munishi na kulia ni Ofisa Uhusiano wa chuo, Leonidas Tibanga

Alisema majengo yaliyokamilika ni ya utawala, kumbi za mihadhara, maktaba na ofisi za wafanyakazi.

Profesa Mjema alisema mpaka kukamilika kwake majengo hayo yamegharimu Sh bilioni 1.46 ambazo zimetokana na mapato ya ndani.

“Napenda kutoa taarifa kwamba ujenzi umekamilika ambapo kwa sasa mazingira ni mazuri kwani miundombinu mipya na ya kisasa inakifanya chuo kutoa huduma kwa ufanisi na tunaomba wadau wajitokeze kuchangia tujenge mabweni ya wasichana,” alisema Profesa Mjema

Alisema wanafunzi wakike wanaishi kwenye mazingira magumu kwani wengi wao wanaanza chuo wakiwa na umri mdogo na ndiyosababu wametoa kipaumbele kwao kujengewa bweni.

Profesa Mjema alisema kilele cha harambee ya kujenga mabweni ya wasichana itafanyika Jumamosi ya tarehe 24 mwezi huu jijini Mbeya na mgeni rasmi atakuwa Spika wa Bunge ambaye ndiye mlezi wake, Dk. Tulia Ackson.

Alisema chuo kimefanya juhudi za kuwafikia wadau mbalimbali zikiwemo taasisi namashirika ya serkali na yasiyo ya kiserikali pamoja na sekta binafsi kuchangia ujenzi huo.

Vilevile, alisema chuo kimeweza kufikisha  jambo  hilo kwa wabunge  kwani pia ni wadau muhimu wa maendeleo ya Elimu nchini.

“Tunawaomba wadau wotewenye mapenzi mema na maendeleo walipo ndani na nje  kutushika mkono  kwa kuchangiachochote ili tuweze kukamilisha harambee pia tukimuunga mkono  mlezi wa Kampasi  ya CBE Mbeya, Dk. Tulia Ackson Spika wa Bunge la Jamhuri wa Tanzania, ambaye niMbunge wa Mbeya Mjini,” alisema.

Aliwashukuru  wadau   ambao   tayari   wamechangia   nawengine kutoa ahadi zao  na kuwataka wanaoweza kuchangia kutumia akaunti ya NMB namba 20601100030 au MPESA 977992.

CBE ina kampasi tatu za Mbeya, Mwanza na Dodoma na yanne ujenzi wake unatarajiwa kuanza mwezi wa 11 baada ya chuo hicho kukabidhiwa eneo na Serikali ya Zanzibar.

error: Content is protected !!