October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Xi hana mpango wa kufanya ziara Saudi Arabia

Xi Jinping, Rais wa China

Spread the love

WAKATI vyombo vya habari vikiripoti kuwa nchi ya Saudi Arabia ipo kwenye maandalizi ya kumpokea Rais wa China Xi Jinping, Waziri wa Mambo ya Nje ya China amekanusha juu ya kuwepo kwa ziara hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Wizara ya Mambo ya Nje ya China imesema kwa sasa hakuna taarifa za kutoa kuhusu ripoti kwamba rais wa nchi hiyo, Xi Jinping atazuru nchi hiyo.

Rais Xi hajawahi kitoka nje ya China kwa ajili ya ziara tangu Januari ya mwaka 2020.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China alisema Alhamisi iliyopita kwamba hakuwa na maelezo ya kutoa kwa sasa alipoombwa kutoa maoni kuhusu ripoti ya vyombo vya habari kwamba Rais Xi Jinping atatembelea Saudi Arabia wiki ijayo.

Gazeti la The Guardian liliripoti kwamba mipango inaendelea nchini Saudi Arabia kwa ajili ya mapokezi makubwa ya Xi, bila kusema ilikopata taarifa hizo.

Xi hajafanya ziara yoyote rasmi katika nchi ya kigeni tangu Januari 2020, mwezi ambao dunia ilianza kukumbwa na ugonjwa wa Uviko-19.

Makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema nchi kama Saudi Arabia, mshirika wa kiuchumi wa Beijing, zimehama kutoka sera ya “kunyamaza” kuhusu unyanyasaji wa Uyghur hadi “kujihusisha”.

Aprili mwaka jana, Xi Jinping alisema kwamba China lazima ifuate sera yake kali ya “kuondoa Uviko” huku ugonjwa huo ikielezwa bado upo katika baadhi ya nchi duniani.

Nchini China pia watu wenye kesi zisizo na dalili au kali sana lazima wawekwe karantini katika vituo vya kati.

error: Content is protected !!