Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali yafuta tozo za miamala ya kielektroniki
Habari za SiasaTangulizi

Serikali yafuta tozo za miamala ya kielektroniki

Dk. Mwigulu
Spread the love

BAADA ya kilio cha zaidi ya mwaka mmoja kutoka kwa Watanzania na wadau mbalimbali, hatimaye Serikali imefuta tozo kwenye miamala ya kielektroniki uamuazi ambao utaanza kutekelezwa tarehe 1 Oktoba mwaka huu. Urumasalu Kisung’uda, TUDARCo… (endelea).

Hatua hiyo inajiri baada ya Chama Cha Mapinduzi  pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan kuamuagiza Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, kufanyia marekebisho tozo hizo na kusikiliza malalamiko ya wananchi.

Uamuzi huo umetangazwa leo tarehe 20 Septemba, 2022 bungeni na Dk. Nchemba baada ya kipindi cha maswali na majibu.

Amesema hatua hiyo itaathiri mapato, lakini serikali itatafuta namna ya kuhakikisha hakutokei athari hizo.

Dk. Mwigulu amesema serikali imefuta tozo za miamala ya benki kwenda kwenye mitandao ya simu kuanzia tarehe 01, Oktoba 2022.

Pia serikali imefuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki kwenda mitandao ya simu (pande zote);

Imefuta tozo ya kuhamisha fedha ndani ya benki moja (pande zote); imefuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki moja kwenda benki nyingine (pande zote);

Amesema wafanyabiashara (merchants) hawatahusishwa kama ilivyo kwenye kanuni za sasa;

Pia Serkali imesema Kusamehe tozo ya miamala kwenye utoaji wa fedha taslimu kupitia wakala wa benki na ATM kwa miamala yenye thamani isiyozidi shilingi 30,000; na

Ameongeza kuwa Serikali imepunguza gharama ya miamala kwa asilimia 10 hadi asilimia 50 kufuatana na kundi la miamala.

“Ikumbukwe kuwa tozo hizo ambapo viwango vya tozo vilishushwa kwa asilimia 30 kutoka kiwango cha juu cha shilingi 10,000 hadi kiwango cha juu cha shilingi 7,000, viwango ambavyo vilianza kutumika tarehe 07 Septemba, 2021. Kadhalika, Mheshimiwa Rais alisisitiza kupunguzwa zaidi tozo ambapo Wizara ya Fedha ilipunguza tozo zaidi kwa kushusha tena kiwango cha juu kutoka 7,000 hadi 4,000,” amesema.

Waziri Mwigulu amesema, baada ya kufutwa kwa tozo hizo, serikali itabana matumzi kwenye maeneo mbalimbali ili kufidia fedha ambazo zingekusanywa kupitia tozo ambazo zimefutwa.

Sehemu hizo za kubana matumizi ni pamoja na safari zisizo za ulazima.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

error: Content is protected !!