Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Waziri Bashungwa awapa neno walimu kuchangamkia fursa NMB
Habari Mchanganyiko

Waziri Bashungwa awapa neno walimu kuchangamkia fursa NMB

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania imewataka walimu kutumia fursa zinazotolewa na Benki ya NMB kujiwekea malengo binafsi na kujiendeleza ilikuboresha Hali ya maisha yao na familia zao. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea.)

Akizindua mpango maalumu kwa ajili ya walimu wa mkoa Kagera, wilaya ya Karagwe, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Tamisemi, Innocent Bashungwa ameipongeza NMB kuanzisha mipango ya kuwakwamua wananchi inayokwenda sambamba na juhudi za Serikali.

Amesema mpango ulioanzishwa na benki hiyo kwa ajili ya mikopo ya kuwainua walimu ikiwa ni pamoja na mikopo ya kujiendeleza kielimu itasaidia kufanikisha mipango mbalimbali ya walimu na makundi mengine.

Bashungwa amesema walimu ni kundi kubwa la waajiriwa ndani ya wizara hiyo na hatua ya NMB kutoa mikopo pia itaboresha ubora wa elimu na walimu kujipatia mitaji kwa ajili ya shughuli zao za kiuchumi na kijamii.

Pia, amesema Serikali itakuwa bega kwa bega na benki hiyo pamoja na Taasisi nyingine ambazo juhudi za kazi zao zinalenga kuyakwamua kiuchumi makundi mbalimbali ya wateja wao.

Naye Mkuu wa Idara ya Biashara za Serikali wa NMB, Vicky Bishubo amesema hatua hiyo imekuja baada ya utafiti kufanyika na kuonyesha kundi la walimu linahitaji kuwezeshwa kwa mikopo kupitia mpango maalumu.

“Tunaamini, walimu hawa tuliowapa elimu leo watasaidia kupeleka elimu watakayoipata hapa kwa wenzao na hata familia zao na jamii kwa ujumla juu ya huduma nzuri zinazotolewa na benki ya NMB, lengo ni kumfanya mwalimu kuwa maisha mazuri wakati wote,” alisema Vicky.

Alisema Mpango wa ‘Mwalimu Spesho’ umejumuisha huduma zote zinazomwezesha mwalimu kupata Mikopo yenye riba nafuu, ikiwemo ya kujiendeleza kielimu yeye na watoto wake, mikopo ya biashara ndogondogo, ujenzi, vyombo vya moto kama Boda boda na Pikipiki za miguu mitatu.

Vicky alisema alitaja mikopo mingine kwenye mpango huo ni bima kujikinga na majanga mbalimbali, mkopo ya pembejeyo na Mashine za kilimo,fursa za kushiriki promosheni na kujishindia zawadi mbali mbali lakini wanatoa elimu ya Kifedha kwa walimu.

Walimu hao kutoka shule mbalimbali za Wilaya hiyo walipatiwa mafunzo na maofisa wa Benki hiyo na kupata nafasi ya kupata maelezo ya kina kuhusu ubora wa mpango huo utakaowanufaisha walimu nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!