Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Polisi Dar wamkamata anayetuhumiwa kumuua mke
Habari Mchanganyiko

Polisi Dar wamkamata anayetuhumiwa kumuua mke

Spread the love

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linamshikilia Selemani Malima, anayetuhumiwa kwa mauaji ya mke wake, Husna Mjaliwa, kwa sababu ya mgogoro wa kifamilia. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumanne, tarehe 19 Julai 2022, na Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, ACP Jumanne Muliro, ikiwa ni takribani mwezi mmoja tangu mtuhumiwa huyo kudaiwa kutoroka  baada ya kufanya mauaji ya mke wake, tarehe 12 Juni mwaka huu.

Kamanda Muliro amesema kuwa, mtuhumiwa huyo alikamatwa tarehe 18 Julai 2022, maeneo ya Mbande jijini Dodoma, alikokuwa amejificha.

“Jeshi la Polisi limemkamata Malima aliyekuwa mkazi wa Keko Mwanga, kwa tuhuma za mauaji ya mke wake Husna  aliyekuwa mkazi wa Goba, kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali tumboni, lililotokea tarehe 12 Juni 2022 na mara baada ya tukio hilo alitoweka,” amesema Kamanda Muliro na kuongeza:

“Baada ya mahojiano ya kina, mtuhumiwa ameonesha kisu alichotumia kumuua mke wake. Uchunguzi wa shauri hili unakamilishwa na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani haraka iwezekanvyo.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!