Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Fedha za Uviko-19 kufikisha maji kwa wananchi milioni moja vijijini
Habari Mchanganyiko

Fedha za Uviko-19 kufikisha maji kwa wananchi milioni moja vijijini

Spread the love

WAKALA wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), umesema kufikia mwishoni mwa mwezi huu miradi maji 172 inayojengwa na fedha za Uviko-19 itakuwa imekamilika na wananchi 1,036,071 kupata huduma ya maji. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Hayo yameelezwa leo Jumanne tarehe 19, Julai, 2022 na Mkurugenzi Mkuu wa Ruwasa, Mhandisi Clement Kivegalo akizungumzia mafanikio ya mamlaka hiyo tangu kuanzishwa kwake na mipango ya mwaka huu wa fedha.

Amesema kupitia mpango wa UVIKO Serikali ilitoa fedha ambapo Ruwasa ilitengewa Sh 78.53 bilioni na  kupitia fedha hizo imetekeleza miradi 172.

“Hadi Juni miradi 68 ilikuwa imekamilika na iliyobaki inatarajiwa kukamila mwezi huu na wananchi 1,036,071,” amesema.

Kivegalo amesema mambo ambayo yalikuwa changamoto katika sekta ya maji vijijini ni gharama kubwa ya ujenzi wa miradi ambayo hata hivyo ilikuwa haitoi huduma.

“Mara nyingi kilio kilikuwa uhalisia wa gharama za kwenye vitabu na mradi unavyoonekana kwa macho,” amesema na kuongeza;

“Tumeona hili ni jambo la kulikabili kwasababu linapunguza kasi ya Serikali kuendelea kuwapatia huduma ya maji wananchi.”

Kutokana na hali hiyo amesema katika mwaka wa fedha uliopita walitangaza zabuni ya miradi 86 na kulipata fursa ya kujadiliana na wakandarasi.

“Bei kabla ya majadilinao ilikuwa Sh367.3 bilioni lakini baada ya majadilinao gharama zilipungua hadi Sh309.9 bilioni   na kuokoa Sh57.4 bilioni,” amesema Mhandisi Kivegalo

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NBC yapata tuzo ya mwezeshaji bora wa mikopo serikali Afrika

Spread the loveBenki ya NBC imepata tuzo ya Mwezeshaji Bora wa Pamoja...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko aipongeza GGML kudhibiti vifo, majeruhi mahali pa kazi

Spread the loveNAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love  BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

error: Content is protected !!