Sunday , 12 May 2024
Home Habari Mchanganyiko NBC yapata tuzo ya mwezeshaji bora wa mikopo serikali Afrika
Habari Mchanganyiko

NBC yapata tuzo ya mwezeshaji bora wa mikopo serikali Afrika

Spread the love

Benki ya NBC imepata tuzo ya Mwezeshaji Bora wa Pamoja wa Mikopo ya Serikali Kuu nchini katika Bara la Afrika kwa mwaka 2023 katika Tuzo za Benki za EMEA. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Tuzo hiyo inalenga kutambua jitihada za Benki ya NBC kama Mwezeshaji Mkuu wa mkopo wa Dola za Kimarekani milioni 200 kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ambapo Benki ya NMB ilikuwa Mkopeshaji mwenza.

Rais wa Zanzibar, Dk. Ally Mwinyi  (katikati) akishududia Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Theobald Sabi  (kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Dk. Juma Malik Akili wakisaini mkataba utakowezesha Zanzibar kupata mkopo wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 200 sawa na shilingi bilioni 470 kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya Zanzibar. Mkopo huo ulitolewa na benki ya NBC ikiwa kama mwezeshaji mkuu kwa kushirikiana na benki ya NMB mwezi Julai mwaka jana.

Fedha hizo zilielekezwa katika kuboresha huduma za kijamii na kuendeleza miundo mbinu muhimu Zanzibar, hatimaye kuboresha ubora wa maisha ya wakazi wake na kuwezesha ukuaji endelevu katika visiwani humo.

Aidha, tuzo hiyo inatajwa kuwa ni uthibitisho wa dhamira ya Benki ya NBC katika uwezeshaji wa miradi endelevu, ikionyesha kujitolea kwake katika kuimarisha jamii inayohudumu.

Kufuatia mafanikio hayo, Theobald Sabi, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, alielekeza shukrani zake kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, wateja wa benki hiyo na wakopeshaji wenza kwa kuamini na kushirikiana nao.

Kwa mujibu wa  Sabi, tuzo hiyo ni utambulisho si tu wa uzoefu wa benki katika shughuli za fedha, bali pia jukumu lake katika kuharakisha mabadiliko chanya na maendeleo katika jamii. 

 “Tuzo hii ni ushahidi wa uwezo wetu katika kurahisisha miamala ya fedha muhimu, pamoja na imani ambayo wadau wetu wametupa. Hii inatupa msukumo wa kuendelea kuboresha huduma zetu ili kuhamasisha maisha endelevu na kujibu mahitaji ya jamii zetu kwa weledi, lengo letu ni kujenga siku za usoni nzuri – hatua kwa hatua,” alisema.

 Tuzo za Benki za EMEA nchini Afrika ni za heshima, zikitambua mafanikio ya kipekee katika sekta ya fedha na kuonyesha ubunifu na umahiri katika masoko ya mtaji barani Afrika. Mafanikio ya Benki ya NBC katika tuzo hizo za heshima yanayathibitisha dhamira yake ya kudumu kwa kuridhisha wateja na maendeleo ya jamii.

 “Kwa zaidi ya miaka hamsini, Benki ya NBC inaendelea kuwa nguzo ya kuaminika katika sekta ya benki nchini Tanzania, ikiwasilisha wigo mpana wa bidhaa na huduma za kifedha ili kutimiza mahitaji mbalimbali ya wateja wake. Mafanikio haya katika Tuzo za Benki za EMEA  ni ushahidi wa kujitolea kwa Benki ya NBC katika kujenga siku za usoni nzuri kwa wote,” Sabi aliongeza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

BiasharaHabari Mchanganyiko

PPAA yajipanga kuwanoa wazabuni namna kuwasilisha rufaa kieletroniki

Spread the loveIli kukabiliana na mageuzi yaliyofanyika katika Sheria mpya ya Ununuzi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

error: Content is protected !!