WAANDAMANAJI wamekusanyika katika kituo cha treni mjini Colombo nchini Sri Lanka kutaka kaimu Rais Ranil Wickremesinghe aondoke madarakani.
Ranil aliteuliwa kuwa rais wa muda wa Sri Lanka baada ya Gotabaya Rajapaska kuimbia nchi hiyo na kwenda uhamishoni ambapo alitangaza kujiuzulu kufuatia maandamano ya miezi kadhaa. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea)
Maandamano yamekuwa yakiendelea Sri Lanka baada ya uchumi wa nchi hiyo kuanguka.
Kaimu rais Ranil, alitangaza hali ya dharura na kumpa mamlaka makubwa ya kuongoza nchi hiyo licha ya maandamano kuongezeka kutaka ajiuzulu.
Bunge la Sri Lanka linatarajiwa kumchagua rais mpya katika muda wa siku mbili.
Waandamanaji wamesema kwamba tangazo la hali ya dharura halitawazuia kuendelea kutaka kuundwa kwa serikali mpya.
Maandamano hayo yanaingia siku ya 100, huku zaidi ya watu milioni 22 wakikabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula, mafuta na dawa tangu mwishoni mwa mwaka uliopita.
Leave a comment