Sunday , 3 December 2023
Home Kitengo Maisha Afya Watanzania watakiwa kupima afya mara kwa mara kudhibiti saratani
Afya

Watanzania watakiwa kupima afya mara kwa mara kudhibiti saratani

Spread the love

INAKADIRIWA kuwa Watanzania 14,028 sawa na asilimia 33.3   kila mwaka hupata ugonjwa kwa saratani. Anaripoti Faki Sosi …(endelea).

Kwa mujibu wa Takwimu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Tafiti za Saratani (IARC) za 2018  endapo jitihada hazijafanyika, idadi hiyo inatajwa  kuwa mwaka 2030 itaongezeka kufikia asilimia 50.

Tafiti hizo zinasema kwenye kundi la watu 100,000 wanaopimwa, watu 76 hugunduliwa na ugonjwa huu.

Taarifa ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road ya mwaka 2021 kwa wagonjwa wa kiume :- Saratani wa Tezi dume ni asilimia 21, Saratani ya Koo asilimia 11.8 , Saratani ya utumbo mkubwa na mdogo asilimia 9, saratani ya mdomo na kinywa asilimia 7.3 kwa upande wa wanawake asilimia 43 ni wagonjwa wa Saratani ya Mlango wa kizazi,  saratani ya matiti asilimia 14.2 huku saratani ya koo asilimia 3.8.

Wataalam wanaeleza kuwa hali hiyo inatokana na mtindo wa maisha lakini changamoto kubwa zaidi watu huchelewa kujigundua kama wanaugonjwa huo ambapo asilimia 80 hugundulika wakiwa wamezidiwa hatua ambayo haitibiki.

Utamaduni wa watu kutopenda kupima afya na kukimbilia kwa waganga wa kienyeji kitendo ambacho wanakiona mabadiliko katika miili yao kunasababisha ugonjwa huu kuwa adui mkubwa.

Dk. Rashid Mfaume leo tarehe 29 Oktoba 2023, akizindua kampeni ya upimaji wa saratani ya matiti na shingo ya kizazi kwa wanawake inayoratibiwa na wanawake wenye asili ya India wanaoishi Dar es Salaam.

Dk. Mfaume ametoa wito kwa wananchi kuwa na tabia ya kupima afya zao kwani ugonjwa huo ukigunduliwa mapema unatibika.

“Kwa wanawake waliofika umri wa miaka 30 tunawashauri wapime kwa mwaka mara moja na wale wenye umri wa miaka 40 wapime mara mbili kwa mwaka tukifanya hivyo tutasaidia kuwaokoa watu wetu” amesema Dk. Mfaume.

DK. Mfaume hakuwaacha wanaume ambapo amewashauri kujenga tabia ya kujua afya zao kwa kuwa nao wanauwezekano wa kupata saratani.

Mwakilishi wa wanawake Wakihindi wanaoishi jijini Dar es Salaam, Anurag Kaur ambao ndio walioandaa kampeni hiyo wakishirikiana na shirika la DGPF amesema kuwa wamejenga utaratibu huo ili kuisaidia jamii.

“Tunakusudia mwakani tuwafikie wananchi wa mikoa mingine hapa nchi ili tuokoe kundi la wanawake” amesema Kuar.

Naye Hadija Matambo amesema mwaka 2018 aligunduliwa kuwa ana saratani kwenye titi lake lakini kwa kuwa aliwahi kufika mapema Hospitali alipona.

“Natoa wito kwa wanawake wenzangu wajitokeze kupima mapema kwa ukigundua mapema unapona wasikimbilie kwa waganga watazidi kujiangamiza” amesema Matambo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

Majaliwa aipongeza GGML mapambano dhidi ya Ukimwi

Spread the loveWaziri Mkuu Kassim Majaliwa ameipongeza Kampuni ya Geita Gold Mining...

AfyaHabari Mchanganyiko

GGML waungana na Biteko kuanika mbinu za mapambano dhidi ya Ukimwi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

AfyaMichezo

GGML yatoa milioni 17 kung’arisha ATF Marathon

Spread the loveKATIKA kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali kukabiliana na maambukizi...

Afya

‘Ambulance’ yawarejeshea tabasamu wananchi Mkuyuni

Spread the loveWananachi wa  Tarafa ya Mkuyuni, Halmashauri ya Morogoro mkoani Morogoro,...

error: Content is protected !!