HOSPITALI ya Taifa Muhimbili inatarajia kuwapeleka nchini India watalaam mbalimbali katika sekta ya afya kwa ajili ya mafunzo ya ugonjwa wa Ini, anaandika Angel Willium.
Watalaam hao ni pamoja na madakatari saba, wauguzi wawili pamoja na mhandishi wa vifaa tiba ambao watakaa huko kwa muda wa miezi mitatu.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma, Aminiel Aligaesha amesema, madakatari hao wanatarajia kuondoka Novemba 29, mwaka huu na watakaporudi wataongeza ufanisi katika kufanya uchunguzi na tiba ya ugonjwa wa Ini na kuondoa uvimbe mkubwa unaodhoofisha afya ya mgonjwa.
“Mafunzo hayo yatachukua miezi mitatu, na watarejea nchini wiki ya kwanza ya mwezi machi mwaka 2018, lengo ni kujenga uwezo wa ndani utakaowezesha upandikizaji wa Ini kwa mgonjwa”amesema Aligaesha.
Aidha, Aligaesha amesema upatikanaji wa huduma hizi hapa nchini, utasaidia kwa kiwango kikubwa kuokoa na kuboresha maisha ya mgonjwa.
Mmoja wa madaktari wanaotarajia kwenda kwenye mafunzo, John Rwegasha ambaye anatibu ugonjwa wa mfumo wa chakula na Ini amesema anashukuru uongozi wa hospitali kuchagua kitengo chao kwenda nchini India.
Leave a comment