Monday , 26 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wadau katiba mpya wamtupia neno Rais Magufuli
Habari za SiasaTangulizi

Wadau katiba mpya wamtupia neno Rais Magufuli

Willium Kahale, Ofisa Programu wa Dawati la mchakato wa Katiba wa LHRC
Spread the love

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC), kimeibuka na kusema kwamba hatma ya katiba mpya ipo mikononi mwa Rais John Magufuli kama atakuwa na utashi wa kweli wa kisiasa, anaandika Nasra Abdallah.

Kadhalika LHRC kimesema ukali wa Rais Magufuli ungependeza zaidi endapo angekuwa anaufanya kwa kufuata katiba ya nchi.

Hayo yamesema leo jijini Dar es Salaam na Ofisa Programu wa Dawati la Mchakato wa Katiba wa kituo hicho, Willium Kahale, wakati wa mjadala wa vyama vya siasa.

Vyama hivyo vimekutana kwa ajili ya kujadili hatma ya mchakato wa kupata katiba mpya hapa nchini.

Kahale amesema mambo mengi anayoyafanya Rais kwa sasa yapo katika rasmi ya katiba, lakini haitakuwa na maana kama mambo hayo hayatakuwepo katika sheria mama ambayo ni katiba .

Ofisa huyu alieleza pia sababu ya kuwakutanisha viongozi hao wa kisiasa kwa sasa ni kutaka kuibua upya madai ya mchakato wa katiba.

“Pamoja na katiba kuwa na umuhimu kwa watu wote hivyo wanasiasa ni wadau wakubwa kwani ili kuepusha machafuko katika chaguzi mbalimbali ni lazima tuwe na katiba nzuri na tungependa kuona inapatikana kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020,”amesema Kahale.

Alivitaka vyama vya siasa kudai katiba mpya kwani wao wana nguvu kubwa ya kuushawishi umma.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Kitaifa ya Ushirikiano wa Maendeleo kwa vijana, Israel Ilunde, amesema ili katiba mpya ipatikane kunahitajika utashi wa Rais na Baraza lake la Mawaziri.

Ilunde amesema ipo haja ya kuitishwa kwa mkutano wa kitaifa kujadili suala la mchakato wa katiba na vyama vya siasa na wadau mbalimbali kuendelea kutoa elimu ya uraia kwa wananchi ili waone umuhimu wa kuendelezwa kwa mchakato huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Hamahama Ngorongoro kutikisa maandamano ya Chadema Arusha

Spread the loveMAELFU ya wanachama na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na...

Habari za SiasaTangulizi

Waliofariki ajalini Arusha kuagwa siku ya maandamano Chadema

Spread the loveMIILI ya watu 25 waliofariki dunia katika ajali iliyohusisha lori...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali kuiburuzwa mahakamani ajali iliyoua 25 Arusha

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), imeitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

error: Content is protected !!