April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Washukiwa 15 mauaji kanisani Sri Lanka wauawa

Spread the love

WATU 15 wanaoshukiwa kuhusika katika shambulio la kigaidi lililopoteza maisha ya watu 253 kwenye makanisa nchini Sri Lanka, wameuawa katika majibizano ya risasi. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Watu hao wanaodaiwa kuwa wanamgambo wa dola la Kiislamu (ISIS) wameuawa huku wengine wakitokomea kusikojulikana  baada ya jeshi la polisi jana kuvamia makazi yao.

Kwa mujibu wa mitandao ya kimataifa, Jeshi la Polisi lilipovamia makazi hayo yaliyoko mashariki mwa Sri Lanka mjini Sainthamaruthu, walikuta milipuko mitatu, sare na bendera za ISIS.

Aifsa wa Polisi Sri Lanka, Meja Jenerali, Aruna Jayasekera   amesema watu sita kati ya 15 waliouliwa ni washukiwa wa moja kwa moja wa tukio hilo lililotokea siku ya Pasaka tarehe 21 Aprili 2019, na wengine tisa ni raia wa kawaida wakiwemo watoto.

Meja huyo amesema, polisi wanaendelea na uchunguzi kuhusu madai ya raia kushirikiana na wanamgambo wa ISIS.

error: Content is protected !!