Saturday , 10 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Prof. Lipumba aunda safu yake mpya ya uongozi CUF
Habari za Siasa

Prof. Lipumba aunda safu yake mpya ya uongozi CUF

Spread the love

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba ameteua Wakurugenzi na Manaibu wakurugenzi wapya. Anaripoti Hamis Mguta…(endelea).

Prof. Lipumba amesema uteuzi huo ni hatua ya kutekeleza majukumu na mamlaka aliyopewa na Katiba ya chama hicho ya 1996 (toleo la 2014) ibara ya 91(1)(f) ambayo inamtaka kuteua wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa, Wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi na Wakurugenzi na Manaibu wake kisha kufikisha mbele ya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa ili kuthibitishwa.

“Baada ya kushauriana na Makamu Mwenyekiti wa chama Zanzibar, Abbas Mhunzi na Makamo Mwenyekiti Tanzania Bara, Maftah Nachuma nawateua Zaynab Amir Mndolwa, Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi na Naibu wake, Omar Mohamed, Habibu Mnyaa, Mkurugenzi wa Mambo ya nje na Naibu wake ni Mohamed Ngululangwa, Mneke Jafar, Mkurugenzi Mipango na Uchaguzi na Naibu wake ni Mohamed Vuai,” amesema.

Viongozi wengine walioteuliwa na Prof. Lipumba ni Abdul Kambaya ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma na Naibu wake Mohamed Salim, Haroub Shamis, Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Sheria na Naibu wake Salvatory Magafu, Thinney Mohammed, Mkurugenzi Mafunzo na Uhamasishaji na Naibu wake Masoud Mhina.

Amesema kwa mujibu wa Katiba ya CUF ya 1992 (toleo la 2014) ibara ya 91(1)(I) amewateua pia Makaimu, Makamo wenyeviti na Makaimu Katibu Watendaji na Manaibu Katibu Watendaji wa Jumuiya ya Vijana JUVCUF ambao ni Hamidu Bobali, Kaimu Mwenyekiti na Kaimu Makamo Mwenyekiti, Faki Khatib, Yusuf Kaiza, Kaimu Katibu Mtendaji na Kaimu Naibu Katibu Mtendaji, Mbaraka Chilumba.

Jumuiya ya wanawake (JUKECUF) amewateua Dhifaa Bakar, Kaimu Mwenyekiti na Kaimu Makamo Mwenyekiti, Kiza Mayeye, Anna Paul, Kaimu Katibu Mtendaji na Kaimu Naibu Katibu Mtendaji Leila Haji.
Kwa upande wa Jumuiya ya Wazee (JUZECUF), Mzaa Chunga, Kaimu Mwenyekiti na Kaimu Makamo Mwenyekiti Hamida Abdallah, Hamis Makapa, Kaimu Katibu Mtendaji na Said Salim, Kaimu Naibu Mtendaji.

Uteuzi huo utafikishwa kwenye kikao cha Baraza Kuu la Uongozi Taifa kwa kuthibitishwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lussu: Mkataba wa DP bandarini si wa miaka 100

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amesema hakuna ukweli wowote...

Habari za SiasaTangulizi

Maulid Mtulia: Kutoka ubunge hadi U-DAS

Spread the love ALIYEKUWA mbunge wa Kinondoni, kupitia vyama vya The Civil...

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

error: Content is protected !!