April 12, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kimbunga cha Keneth: Mtwara, Lindi yapumua

Spread the love

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imewataka wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara kuendelea na shughuli zao, huku ikiwatahadharisha kufuatilia utabiri utakaotolewa kila mara kuhusu Kimbunga Kenneth. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kauli hiyo ya TMA imekuja baada ya Kimbunga Kenneth kilichotabiriwa kutokea katika mikoa hiyo Alhamisi ya terehe 25 Aprili 2019 na kuleta athari, kubadili mwelekeo wake na kwenda katika maeneo ya Kusini mwa Pwani ya nchi ya Msumbiji.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana tarehe 26 Aprili 2019, Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agnes Kijazi, amesema kimbunga Kenneth bado kipo katika ardhi ya Msumbiji na mwishoni mwa wiki kinatarajiwa kurudi baharini.

Dk. Kijazi amesema kimbunga hicho kitakaporejea baharini kinaweza leta athari katika mikoa hiyo kama ilivyotabiriwa awali na TMA. Hata hivyo, amesema mamlaka hiyo itaendelea kufuatilia kwa ukaribu kimbunga hicho na kutoa taarifa kwa umma.

error: Content is protected !!