Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Wapalestina waanza kukimbia Gaza baada ya tishio la Israel
Kimataifa

Wapalestina waanza kukimbia Gaza baada ya tishio la Israel

Spread the love

WAPALESTINA waishio katika Ukanda wa Gaza, wameanza kukimbia makazi yao baada ya Israel kuwapa saa 24 wakitaka wahamie sehemu nyingine ili kupisha mashambulizi yake. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Mtandao wa BBC Swahili umeripoti kuwa, leo Ijumaa, wananchi wa Gaza wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 1,000,000, baadhi yao wameanza kupakia mizigo yao na kuhakama kueleka kusini walikoamriwa kwenda kupata hifadhi na Israel.

Israel ilitoa agizo hilo kwa raia wa Gaza kuyahama makazi yao, ikiwa ni muda mfupi tangu isitishe kupeleka huduma muhimu kwenye eneo hilo ikiwemo chakula, mafuta na umeme.

Pia, imeahidi kufanya mashambulizi mfululizo hadi pale kundi la wanamgambo la Hamas la Palestina, litakapowaacha watu zaidi ya 100 waliowaweka mateka.

Wakati hayo yanajiri, Umoja wa Mataifa (UN), umesema wananchi wa Gaza wanakabiliwa na hali ngumu ya kimaisha baada ya kukosa huduma muhimu, huku wajawazito 50,000 wakitajwa kuwa hatarini kufuatia mapigano yanayoendelea.

Tayari ofisi ya UN ya kuratibu  masuala ya kibinadamu,  imetoa wito kwa nchi wanachama kutoa msaada wa Dola za Marekani 294 milioni, kwa ajili ya kuwapa mahitaji ya dharura Wapalestina.

Mpaigano hayo yameibuka baada ya Hamas kufanya shambulio la kushtukiza upande wa Israel, liliopoteza maisha ya watu 900 waliokuwemo katika sherehe. Kufuatia shambulizi hilo, Israel imeendelea kufanya mashambulizi kulipa kisasi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

error: Content is protected !!