Wednesday , 8 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Wanandoa mbaroni kwa utapeli wa bilioni 14, ni kupitia sarafu ya kidijitali
Kimataifa

Wanandoa mbaroni kwa utapeli wa bilioni 14, ni kupitia sarafu ya kidijitali

Spread the love

JESHI la Polisi nchini Sri Lanka limeanzisha uchunguzi kuhusu udanganyifu mpya wa fedha ambao hadi sasa umehusisha utapeli wa Sh bilioni 14 huku watu 8,000 wakiwa waathirika katika mpango wa sarafu za kidijitali (cryptocurrency). Anaripoti Mwandishi wetu … (endelea).

Msemaji wa polisi nchini humo, SSP Nihal Thalduwa amesema kuwa ulaghai huo unaodaiwa kufanywa na wanandoa wa China na raia wa Sri Lanka, umenza tangu 2020 ambapo watu 8,000 wametapeliwa.

Msemaji huyo amesema washukiwa hao walikuwa wakiwashawishi watu kuwa wakiwekeza katika sarafu ya crypto watapata faida kubwa.

Amesema wanandoa hao ndio waanzilishi wa ulaghai huo na walifanya wahanga hao kuwaamini kwa kuwaalika kwenye chakula cha heshima  cha jioni.

Uchunguzi huo unaofanywa na Idara ya Upepelezi ya Makosa ya Jinai (CID) ya Jeshi hilo imegundua kuwa matapeli hao waliwazuia wawekezaji waliowanasa kwenye mtego wao kutotoa faida zao walizopata kwenye uwekezaji huo.

“Wawekezaji hao walipojaribu kuondoa faida waliyopata kupitia uwekezaji huo, washukiwa hawakuwaruhusu kutoa fedha hizo” amesema SSP Thalduwa.

SSP Thalduwa amesema malalamiko kadhaa yamepokelewa katika kitengo cha Udanganyifu wa Kifedha cha CID.

“Baada ya uchunguzi wa muda mrefu, tuwakamata wenzi hao wa Kichina kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bandaranaike walipojaribu kutoroka nchini. Wanandoa hao wa China kwa sasa wako rumande,” amesema na kuongeza kuwa;

Mshukiwa wa raia wa Sri lanka alikamatwa tarehe 11 Oktoba, 2022 na baadaye akaachiwa kwa dhamana baada ya kufikishwa kortini.

Jeshi hilo limekamata washukiwa wengine ambao wanaendelea kuwapeleleza juu ya tuhuma hizo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!