Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mkurugenzi wa Bodi TMA aipongeza kwa kutekeleza mikataba ya Baraza la Wafanyakazi
Habari Mchanganyiko

Mkurugenzi wa Bodi TMA aipongeza kwa kutekeleza mikataba ya Baraza la Wafanyakazi

Spread the love

 

MWENYEKITI  wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Buruhani Nyenzi ameipongeza TMA kwa kutekeleza Mkataba waBaraza kwa kuhakikisha wajumbe wa Baraza wanakutana mara mbili kwa mwaka. Anaripoti Mwandishi Wetu, Pwani … (endelea).

Alieleza hayo wakati akifungua rasmi Baraza la Wafanyakazi wa TMA la pili kwa mwaka 2022 katika Ukumbi wa Manesi na Wakunga, Kibaha, Pwani, leo tarehe 29 Oktoba, 2022.

Taarifa ya Mwenyekiti wa Baraza, nimeelezwa kuwa hiki ni kikao cha pili, hivyo anaipongeza Mamlaka kwa kuwa na mabaraza mawili kwa mwaka kulingana na Mkataba.

Dk. Nyenzi aliendelea kwa kuipongeza Mamlaka kwa utekelezaji mzuri wa miradi mikubwa namafanikio yaliyopatikana hususani fanikio la kuboresha miundo mbinu ya hali ya hewasambamba na kutekeleza agizo la Serikali la kuhamia Dodoma, Makao Makuu ya nchini.

Vilevile, aliishukuru Bodi kwa kazi nzuri ya usimamizi waTaasisi uliochangia mafanikio hayo.

Nitumie fursa hii kuwashuruku wajumbe wa Bodiambao  nimefanya nao kazi kwa kipindi cha miakamitatu kwa utumishi wao uliotukuka uliopelekeamafanikio yote haya yaliyoainishwa na Mwenyekitiwa Baraza hili, ikiwa ni pamoja na uboreshaji wamaslahi ya wafanyakazi,” alieleza Dkt. Nyenzi

Mkurugenzi TMA, Dk. Agnes Kijazi

Awali, Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi Dk. Ladislaus Chang’a, akisoma taarifa ya Mwenyekiti wa Baraza kwa niaba ya Dk. Agnes Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu wa tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), alishukuru Serikali kupitia Wizara na Bodi ya TMA kwa ushirikiano na kazi kubwa iliyofanyika yakufanikisha malengo ya Taasisi, ambapo viwango vya usahihi wa utabiri vimeendelea kuongezeka, nakutoa wito kwa watanzania kutumia taarifa hizoza hali ya hewa.

Katika taarifa hiyo, Dk. Kijazi aliendelea kueleza kuwaDhumuni kuu la Baraza hili ni kufanyatathmini ya utendaji wa Mamlaka ambao utasaidiakuongeza ubora na ufanisi katika utoaji wahuduma kwa umma kwa lengo la kupunguza athariza mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi”.

Akielezea baadhi ya mafanikio yaliyopatikanakatika kipindi cha Baraza lililopita na Baraza la sasa, Mwenyekiti wa Baraza alisema mafanikiohayo ni pamoja na ufanisi wa utekelezaji washeria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa na Kanunizake, ununuzi wa rada na miundo mbinu kwa ujumla, uboreshaji wa maslahi ya wafanyaki kwakuendelea kupandishwa vyeo, kubadilishwakada,ongezeko la mishahara na kuhuishwa kwa miundo ya kada kwa watumishi kufuatia mabadiliko ya Miundo ya Maendeleo ya Watumishi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

Habari Mchanganyiko

Mfanyakazi CRDB atoa sababu za kubambikiwa kesi, hukumu Mei 30

Spread the love  MFANYAKAZI wa Benki ya CRDB, Ibrahim Masahi (40) ameieleza...

Habari Mchanganyiko

Waziri Ummy atangaza Tanzania kuwa kitovu cha utalii tiba

Spread the loveSERIKALI imesema imedhamiria kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha matibabu ya...

error: Content is protected !!