November 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Morrison aibeba Yanga mbele ya Geita

Spread the love

BAO la mkwaju wa penalti ambalo limefungwa na winga machachari, Bernard Morrison wa klabu ya Yanga katika dakika ya 45 limetosha kuwaandikia Wana-jangwani hao  rekodi ya kufikisha michezo 45 ya ligi bila kufungwa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Katika mchezo huo uliopigwa leo tarehe 29 Oktoba, 2022 kwenye dimba la CCM Kirumba mkoani Mwanza, Yanga wamewalamba matajiri wa dhahabu Geita Gold bao 1-0 ikiwa ni mwendelezo wa Ligi Kuu  Bara.

Penalti hiyo ilipatikana mnamo dakika ya 45 baada ya Heritier Makambo kupiga krosi ambayo mpira ulimgonga kwenye mkono winga wa Geita Gold, Raymond Masota na mwamuzi Frolentino Zabroni kuamuru pigo la penalti ambayo ilizamishwa kimyani na Bernad Morrison huku akimuonyesha kadi ya njano, Masota.

Yanga ambayo imepumzisha baadhi ya mastaa wao wa kikosi cha kwanza walitawala dakika 45 za kipindi cha kwanza na kutengeneza mashambulizi kwenye lango la Geita Gold.

Aidha, katika dakika ya 44, mashabiki wa Yanga walisimama majukwaani na kumpongeza kwa kumpigia makofi Kocha wa timu hiyo kwa, Nasredinne Nabi kwa kuiongoza katika mechi 44 za Ligi bila kufungwa.

Wakati shangwe hilo la mashabiki halijaisha na kuendelea kukaa kwenye viti vyao, Yanga ndipo walipopata penalti iliyoibua utata kutokana na  picha za marudio kuonyesha ilikuwa nje ya boksi.

error: Content is protected !!