Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Wananchi Ileje waiangukia serikali ukamilishaji wa zahanati
Afya

Wananchi Ileje waiangukia serikali ukamilishaji wa zahanati

Spread the love

Wananchi wa kijiji cha Mbembati kata ya Lubanda wilaya ya Ileje mkoani Songwe wamejenga zahanati ya Kijijini hapo kwa nguvu zao ili kupunguza adha ya kusafiri umbali wa kilomita nane kufuata huduma katika kituo cha afya Lubanda. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe…(endelea).

Wananchi hao walianza ujenzi wa zahanati hiyo mwaka 2014 kwa lengo la kuwapunguzia akina mama wajawazito ambao walikuwa wakijifungulia njiani na majumbani wakati wakifuata huduma ya uzazi kituo cha afya Lubanda ambapo awali ilikuwa zahanati.

Akisoma taarifa ya kijiji, Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Odeni Kandonga  amesema kati ya fedha hizo wananchi wamechangia milioni 15.6, fedha ya mfuko wa jimbo ni milioni nne, na michango ya wahisani ni Sh 800,000.

Akijibu ombi la wananchi wa kijiji hicho Mkuu wa Wilaya hiyo, Farida Mgomi amewapongeza wananchi kwa kutumia nguvu zao kushiriki ujenzi huo kwa kuchangia fedha na kuahidi kuwa zahanati hiyo itakuwa  ni mwarobaini wa kupata huduma za afya karibu pindi itakapoanza kutoa huduma

“Kutokana na mwitikio wenu Serikali itahakikisha inawaunga mkono kumalizia sehemu iliyobaki hivyo basi mhandisi wa ujenzi atakuja wiki ijayo kufanya tathmini ya eneo la zahanati ilipobaki ili jengo hilo liingizwe kwenye bajeti kwa ajili ya kutenga fedha za kukamilisha na huduma zianze kutolewa,” amesema Mgomi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

Songwe katika mikakati ya elimu ya lishe kudhibiti udumavu

Spread the love  SERIKALI mkoani Songwe imejipanga kuendelea kutoa elimu ya lishe...

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

error: Content is protected !!