September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waliopona corona duniani milioni 3.1, vifo 388,353

Spread the love

WAGONJWA  wa virusi vya corona (COVID-19) waliopona duniani wafikia 3,183,578 huku vifo vikiwa 388,353. Unaripoti mtandao wa Worlometer … (endelea).

Hadi kufikia leo Alhamisi tarehe 4 Juni 2020, mtandao huo ulikuwa umeripoti wagonjwa 6,591,124 duniani.

Marekani imeendelea kuwa taifa linaloongoza maambukizo ulimwenguni, likiwa na wagonjwa 1,902,031, waliopona 688,670, huku vifo vikifikia 109,146.

 Brazil ina wagonjwa 584,562, waliofariki dunia 32,568 na waliopona wakiwa 266,132.

China ambako ndiko corona ilianzia mwishoni mwa mwaka 2019, ina wagonjwa 83,022, waliofariki wakiwa 4,634 na waliopona wakiwa 78,319 huku wagonjwa wanaoendelea na matibabu nchini humo wakiwa 69 na watatu wakiwa katika hali inayohitaji uangalizi.

error: Content is protected !!