Tuesday , 7 May 2024
Home Kitengo Biashara Wafanyabiashara Tunduma watoa dukuduku ujenzi soko la bilioni 1.9
Biashara

Wafanyabiashara Tunduma watoa dukuduku ujenzi soko la bilioni 1.9

Spread the love

WAFANYABIASHARA katika soko la Majengo halmashauri ya mji Tunduma wameio na Serikali iharakishe ujenzi soko jipya ili waweze kuendelea na zao katika maeneo rafiki na salama kwa bidhaa zao.

Pia wameiomba Serikali kuwawekea mazingira rafiki katika eneo la muda lililotengwa kwa ajili yao ambapo wanatarajia kuhamia ili kupisha ujenzi huo wa soko jipya la ghorofa. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe…(endelea).

Viongozi wa Soko la Majengo wakiteta jambo baada ya ujio wa Sh 1.9 bilioni za kujenga soko la kisasa.

Hayo yamebainishwa leo tarehe 27 Juni 2023 kwa nyakati tofauti walipozungumza na MwanaHALISI Online kuhusu ujenzi wa soko jipya unaotarajiwa kugharimu Sh 1.9 bilioni.

Wamesema mazingira wanayofanyia biashara kwa sasa ni chakavu hali inayowafanya baadhi ya wananchi kutokwenda kununua bidhaa katika soko la sasa.

Mfanyabiashara Joseph Mgode licha ya kuipongeza Serikali kwa kutoa fedha hizo za ujenzi wa soko hilo jipya, ameomba eneo la muda wanakohamia wawekewe miundombinu rafiki ikiwemo vyoo, maji, taa na uzio.

Amesema eneo wanakotarajiwa kuhamishiwa kuna mfereji unaotenganisha nchi ya Tanzania na Zambia hali inayohatarisha usalama wao kwani hujificha vibaka wengi wanaopora vitu.

Naye mjasiriamali Zabera Samson amesema soko la ghorofa litakapokamilika litavuta wateja wengi wa ndani na nje ambapo wataingiza fedha za kigeni na kuwa kimbilio la wengi hasa akina mama wajane wanaopanga bidhaa chini.

Katibu wa soko hilo, Msafiri Lubava amesema siku ya kwanza uliitishwa mkutano eneo hilo ukiongozwa na Mwenyekiti wa halmashauri, Ayoub Mlimba; Diwani, Frank Mponzi na kuwaelezea ujenzi wa soko jipya hivyo wanatakiwa kuhamia eneo la wazi kwa muda.

Afisa  biashara wa halmashauri hiyo, Charles Mazengo amesema wamebahatika kupata fedha hizo kwa ufadhili wa Jumuiya ya Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA).

Alisema ujenzi wa soko hilo litakalokuwa karibu na mpaka wa Tanzania na Zambia, utawakomboa wafanyabiashara na wa Tanzania, Zambia, Malawi na nchi zingine na kuongeza mapato ya Serikali na wafanyabiashara.

Mhandisi wa halmashauri hiyo, Ally Tinga alisema litakuwa soko la kisasa litakaloongeza thamani ya bidhaa za wafanyabiashara, wanaopanga bidhaa chini wataanza kuuzia kwenye vizimba.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi, Afisa mipango wa halmashauri hiyo, Braun Galigo amesema wamepokea fedha Sh 1.9 bilioni kutoka nchi wanachama – Comesa kujenga soko la ghorofa litakalokuwa na fremu za maduka, vizimba zaidi ya 2,000.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

Biashara

Cheza kwa kuanzia Sh 400 kushinda mgao wa Expanse Tournament kasino 

Spread the love  UKISIKIA bosi kacheka ujue Maokoto yanafuatia, Kupitia promosheni pendwa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

error: Content is protected !!