Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Vyuo vikuu Tanzania vyatakiwa kupitia mitaala
Elimu

Vyuo vikuu Tanzania vyatakiwa kupitia mitaala

Naibu Waziri wa Elimu, Omary Kipanga
Spread the love

 

WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania, imevitaka vyuo vikuu na taasisi zingine za elimu kufanya mapitio ya mitalaa ili iweze kuendana na mahitaji ya soko la ajira. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Pia, vyuo hivyo vimetakiwa kuweka mikakati ya kuzalisha wataalamu wa kutosha hususani katika sekta adimu na zenye tija kwa maendeleo ya nchi yetu ili kufikia lengo la kitaifa la kuwa na wahitimu 98,000 kwa mwaka ifikapo 2025/26.

Wito huo umetolewa jana Jumamosi, tarehe 31 Julai 2021 na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Omary Kipanga wakati akifunga Maonesho ya 16 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yalianza 26 Julai.

Kipanga amesema, idadi ya wanafunzi wa shahada ya kwanza kwenye vyuo vya elimu ya juu imeongezeka kutoka 65,064 mwaka 2015/16 hadi 87,934 mwaka 2020/21.

Amesema, wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu wakiongezeka kutoka wanafunzi 125,126 mwaka 2015 hadi 132,392 mwaka 2020.

Naibu waziri huyo amesema, ili mitaala iandane na majitaji ya soko la ajira ni lazima
kuweka msisitizo katika masomo ya sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati (STEM), pamoja na utoaji wa mafunzo kwa vitendo.

Katika hafla hiyo, Kipanga alisema, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita sekta ya elimu ya juu imepata mafaniko makubwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo eneo la udahili na uimarishaji mifumo ya wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu.

Alisema vyuo vikuu vinapaswa kutoa elimu bora ya kiushindani ndani na nje ya nchi, mifumo ya uthibiti ubora “imeendelea kuimarishwa ikiwemo mifumo ya ukaguzi na ufuatiliaji na mifumo ya uhakiki na utambuzi wa sifa za kitaaluma za wahitimu wa elimu ya juu zilizotolewa na vyuo vya nje ya nchi.”

“Pamoja na mafaniko hayo makubwa pia tumeboresha miundombinu ya kufundishia na kujifunzia katika ngazi zote za elimu ikiwemo ujenzi na ukarabati wa madarasa, kumbi za mihadhara, maabara, maktaba, hosteli na ununuzi wa vifaa vya utafiti, pamoja na vifaa vya kufundishia na kujifunzia,” alisema Kipanga.

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof. Charles Kihampa alisema, maonesho ya mwaka 2021 yamekuwa na mafanikio makubwa kwa kupata washiriki wengi na kwamba zaidi ya waombaji 52,000 wa shahada ya kwanza wametuma maombi katika vyuo mbalimbali na kati ya maombi hayo mengine yamefanyika moja kwa moja kupitia maonesho.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanafunzi waliohitimu kidato cha sita ambao wangependa kujiunga na vyuo vya elimu ya juu, wameipongeza TCU kwa kufanya maonesho hayo kwa kuwa wamepata fursa ya kukutana na vyuo vyote katika eneo mmoja na kufanyiwa udahili bila gharama yoyote.

Maonesho ya 16 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoanza Julai 26 na kuhitimishwa Julai 31 yalikuwa na kauli mbiu isemayo “Kuendelea Kukuza na Kudumisha Uchumi wa Kati kupitia Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia”.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari Mchanganyiko

Ugawaji taulo za kike watajwa kutokomeza utoro shuleni

Spread the loveBAADHI ya wanafunzi na walimu wa shule za sekondari mkoani...

ElimuHabari za Siasa

MbungeCCM ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the love  MBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze...

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

error: Content is protected !!