MICHUANO ya klabu kwa ukanda wa Afrika Mashariki na kati (CECAFA Kagame Cup) yataanza kutimu vumbi rasmi kesho kwa jumla ya timu tisa kushiliki. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)
Katika ufunguzi wa michuano hiyo itapigwa michezo miwili ambapo mchezo wa afunguzi utakuwa kati ya Express ya Uganda dhidi ya Atlabara FC utakaochezwa majira ya saa 7 mchana, kwenye dimba la Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.
Mchezo wa pili, utawakutanisha klabu ya Soka ya Yanga ambao utapigwa majira ya saa 10 jioni, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, dhidi ya Big Bullet FC.
Timu hizo tisa zinazoshiriki michuano hiyo, zimegawanyika kwenye makundi matatu, ambapo kila kundi litakuwa na timu tatu.
Michuano hiyo pia itaendelea Agost 2, ambapo wawakilishi wengine kutoka Tanzania klabu ya Azam FC watashuka dimbani dhidi ya KCC kutoka Uganda, mchezo utakaopigwa Azam Complex Chamazi, huku mchezo wa kwanza utakuwa kati ya Message Ngozi na KMKM.
Michuano hiyo itafika tamati Agosti 14 kwa kupigwa mchezo wa fainali, majira ya saa 10 jioni kwenye dimba la Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.
Leave a comment