Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko ‘Viongozi wasitumia miradi kuhalalisha tozo’
Habari Mchanganyiko

‘Viongozi wasitumia miradi kuhalalisha tozo’

Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maaskofu na Mashehe ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Madhehebu ya Dini nchini Askofu William Mwamalanga
Spread the love

VIONGOZI wa dini wamewataka viongozi wa serikali kuacha kutumia kigezo cha ujenzi wa  miradi ya afya, elimu, maji na mingine, ili kuhalalasha tozo ambayo imeibua malalamiko kila kona ya nchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endele).

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 5 Septemba, 2022 na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maaskofu na Mashehe ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Madhehebu ya Dini nchini Askofu William Mwamalanga alisema viongozi hao hawakubaliana mfumo huo kwa kuwa unaumiza wananchi.

Askofu Mwamalanga alisema walikuwa na kongamano lililoshirikisha viongozi wa dini na kutoka na kauli ya moja ya kupinga tozo kwa kuwa inaonekana ni kuwalipisha wananchi kodi mara mbili.

Alisema kinachosemwa na viongozi hao na kinachoonekana mitaani ni vitu tofauti hivyo kuwataka viongozi hao kufikiria njia nyingine ya kupata fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi.

“Baadhi ya mawaziri wamekuwa wakitumia hoja ya utekelezaji wa miradi kama sababu ya kuwepo kwa tozo, ila ukipia huko mitaani hali ni tofauti miradi haitekelezwe, lakini kubwa zaidi ni ugumu wa maisha kwa sasa,” alisema.

Askofu Mwamalanga alisema tozo haziwezi kujenga nchi  kwani tafsiri ya tozo ni sawa na kumnyang’anyi watu ambao hawana sifa ya kutozwa tozo hizo.

“Unapoweka tozo maana yake huchagui mchangiaji awe mlemavu wa kuona, kusikia, viungo au maskini yoyote lazima alipe kama anatumia simu, hii sio sawa,” alisema.

Alisema wanachokiona kwa sasa ni kujenga taifa la waongo wanaongoza wananchi kwa ndimi za udanyifu na kutengeneza uchumi wa kiini macho  kila uchao.

Mwamalanga  amemuomba Rais    Samia Suluhu Hassan, kutumia wataalam wa uchumi kutoka Zambia  ili waje wasaidie kufufua uchumi  wa madini, mifugo, uvuvi na sekta nyingine ambazo hazitumiki ipasavyo, ili kuachana na tozo.

Alisema kutokana na Zambia kuwa na mipango mizuri  wafanyabiashara wakitanzania wanaenda kuwekeza katoka nchi hiyo, hali ambayo imesababisha fedha yao kuwa na thamani kuliko ya Tanzania kwa muda mfupi wa uongozi wa Rais Hakainde Hichilema.

Askofu Mwamalanga alisema Tanzania inapitia changamoto za kiuchumi kutokana na aina ya viongozi ambao wamepewa fursa ya kuongoza sekta nyeti kukosa uadilifu na ubunifu.

“Huwezi kujenga nchi kwa kunyanganya watu wako fedha mifukoni. Kusema kweli hawa wasaidizi wa Rais Samia wanaofikiria tozo hawawezi kukuza uchumi, ni vema wapumzike, ili waweze kumpa nafasi Rais Samia kufanya uteuzi mwingine,” alisema.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

error: Content is protected !!