Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Vigogo watatu Mbozi kikaangoni, TAMISEMI yatoa maagizo
Afya

Vigogo watatu Mbozi kikaangoni, TAMISEMI yatoa maagizo

Spread the love

NAIBU Katibu Mkuu wa TAMISEMI, Dk Charles Mahera amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Abdallah Nandonde kuwasimamisha kazi Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Mbozi-Vwawa, Mganga Mfawidhi na Mfamasia wa hospitali hiyo ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za upotevu wa dawa na kushindwa kusimamia huduma. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe …(endelea).

Dk. Mahera alitoa maagizo hayo leo tarehe 14 Julai 2023 wakati akizungumza na watumishi wa afya katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe baada ya kuhitimisha ziara ya kutembelea na kukagua vituo vya afya na hospitali katika mkoa huo.

Waliosimamishwa ni pamoja na Dk. Nelson Mponjoli ambaye ni Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Mganga Mfawidhi Dk. Keneth Lesilwa na Mfamasia Jeremia Nnko.

Amesema kuwa watumishi hao wanapisha uchunguzi wa mapungufu yaliyobainika katika hospitali hiyo, huku akiagiza uchunguzi kufanyika kwa muda mfupi na kuzingatia haki.

“Watu watatu hao wasimamishwe, uchunguzi ufanyike ndani ya muda mfupi tupate taarifa. Tunaposema tunakusimamisha hatujasema tunakufukuza kazi, tunapomsimamisha isichukue muda mrefu. Ufanyike uchunguzi wa haraka ili mtu aweze kupata stahiki yake. Fanyeni uchunguzi wa haraka bila upendeleo” amesema Dk Mahera.

Amesema kuwa wamefanya uchunguzi kwenye baadhi ya dawa katika hospitali hiyo na kukuta baadhi ya dawa zina  kasoro.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

AfyaHabari Mchanganyiko

Songwe katika mikakati ya elimu ya lishe kudhibiti udumavu

Spread the love  SERIKALI mkoani Songwe imejipanga kuendelea kutoa elimu ya lishe...

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

error: Content is protected !!