Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Biashara Kilombero walilia miundombinu kilimo cha umwagiliaji
Biashara

Kilombero walilia miundombinu kilimo cha umwagiliaji

Spread the love

CHAMA  Cha Mapinduzi  (CCM)  Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro, kimeiomba serikali kujenga miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji kwa ajili ya kukuza uzalishaji wa zao la mpunga na miwa wilayani nchini. Anaripoti Victor Makonda, Morogoro …(endelea).

Ombi hilo limetolewa leo Ijumaa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kilombero, Mohamed Msuya wakati akizungumza na MwanaHALISI Online katika Mji Mdogo wa Mang’ula wilayani Kilombero.

Msuya amesema kuwa wilaya hiyo imejaaliwa ardhi kubwa yenye rutuba na ifaayo kwa kilimo cha mazao ya aina mbali mbali hususani Mpunga na miwa huku changamoto ikiwa ni ukosefu wa miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji. 

“Wilaya ya Kilombero imejaaliwa kuwa na ardhi yenye rutuba, watu wenye ari ya kufanya kazi, changamoto ni ukosefu wa miundombinu ya umwagiliaji hali inayopelekea wakulima kulima kilimo kisicho na uhakika wa kuuvuna kwa kutegemea misimu ya mvua,” Amesema Msuya.

Msuya amesema kuwa karne hii ya Sayansi na Teknolojia, kutegemea mvua kwa ajili ya kuendesha shughuli za kilimo, sio tu kunapunguza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara bali pia kunafifisha kasi ya maendeleo. 

“Ninamuomba Mwenyekiti wangu wa Taifa wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan, kupitia Wizara ya kilimo itujengee miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji kwani vyanzo vya maji vipo vya kutosha, ardhi ipo na watu wenye jitihada za kufanya kazi wapo,” amesema Msuya.

Msuya ameongeza kuwa Kilombero ikijengewa miundombinu ya umwagiliaji ni wazi kuwa itakuwa kitovu kikubwa cha uzalishaji wa mazao yatakayokuza uchumi wa watu wa Kilombero na kuchangia katika ukuaji wa pato la Taifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Cash Days Promo mamilioni yanakusubiri, cheza kupitia Meridianbet kasino 

Spread the love  JIANDAE kwa mshangao wa kustaajabisha Meridianbet kasino ya mtandaoni...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

error: Content is protected !!