RAIS wa Kenya William Ruto amedai kuwa aliyekuwa mtangulizi wake Uhuru Kenyatta anajaribu kubomoa serikali yake kwa kufadhili maandamano. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).
Akizungumza katika ziara yake kwenye Mji Mai Mahiu nchini humo, Ruto alidai kuwa Uhuru alikuwa anafadhili vijana wa Mungiki kusababisha vurugu wakati wa maandamano ya Azimio la Umoja One Kenya Coalition Party.
Ruto alionya kuwa ikiwa rais huyo wa zamani hatasitisha ufadhili wa shughuli za Azimio, atalazimika kuchukua hatua dhidi yake.
Ruto alimtaka rais wa zamani kuwa mwanamume, akidai kwamba walimuunga mkono alipokuwa kwenye uongozi wa nchi.
Kiongozi huyo wa taifa alimtaka Uhuru aache kujiunganisha na kiongozi wa ODM, Raila Odinga, ambaye aliahidi kumzuia kwenye makazi yake ya mashambani.
“Nataka pia kumwomba rafiki yangu Uhuru ajiweke mbali na yule Mzee (Raila). Acha kumpa pesa ya kuajiri Mungiki kuharibu Nairobi. Wewe ulikuwa rais, kuwa mwanamume. Tulikusaidia ulipokuwa rais. Ikiwa hautajitenga naye, tutakutuma mbali pia, kama vile huyo mtu wa mafumbo,” alisema Ruto.
Leave a comment