Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia ataka kibano viongozi wanaotumia madaraka vibaya
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataka kibano viongozi wanaotumia madaraka vibaya

Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan, ameshauri sheria itakayowabana viongozi wanaotumia madaraka yao mabaya vibaya itungwe, ili kuimarisha mfumo wa haki jinai nchini. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Mkuu huyo wa nchi ametoa agizo hilo leo tarehe 15 Julai 2023, baada ya kupokea taarifa ya tume aliyounda kuangalia jinsi ya kuboresha taasisi za haki jinai, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais Samia amesema kwa sasa sheria inatoa mwanya kwa baadhi ya viongozi kutumia madaraka yao mabaya, hususan baadhi ya wanaojaribu kulinda wanaofanya makosa, kitendo kinachopelekea uovu kutokukoma.

“Inabidi itungiwe sheria kwa wale wanaoingia kwenye maeneo siyo ya kwao na wenyewe washughulikiwe vipi. Tunaona kweli kuna matumizi mabaya ya madaraka, wakati mwingine kesi iko kwa DPP lakini atapigiwa simu futa hiyo kesi. Sababu anaweza kufuta kesi bila kutoa sababu na ameshapigiwa simu anafuta ile kesi,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema “kwa hiyo ule udhaifu, uovu ambao kesi ilishtakiwa unaendelea, lakini aliyefutiwa kesi anasema atanigusa nani. Zile kesi za kodi zinafutwa udhaifu unaendelea.”

Kuhusu taarifa aliyopokea, Rais Samia ameagiza mapendekezo yaliyomo ndani yake yafanyiwe kazi mara moja, huku akiagiza tume hiyo inayoongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu, Othman Chande, iendelee kushirikiana na vyombo vya haki jinai katika utekelezaji wake.

“Nataka hii ripoti maeneo yake yatekelezwe kikamilifu, ndiyo maana tukaivunje vipande vipande tume tuingie kwenye sekta zilizotajwa. Kamati gani inakwenda kushughulika na Jeshi la Polisi tu, TAKUKURU na Mamlaka ya Dawa za Kulevya.,” amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia  ameagiza mifumo itakayounganisha vyombo vya haki jinai uanzishwe mara moja ili kuondoa changamoto za utendaji wake ikiwemo ubambikizaji kesi kwa wananchi.

“Vyombo vya haki jinai lazima visomane, kuanzia mtu anavyokamatwa, anavyokwenda kufanyiwa upelelezi vyote vionekane hivyo na jaji anavyotoa hukumu afanye follow up, ndipo haki itakapopatikana vinginevyo utaambiwa saini hapa statement ilishaandikwa, hapa kunatakiwa fedha nyingi sana na tumeweza kwenye eneo la mahakamasi haba na vingine tuviwezeshe hili nalo lifanyike haraka,” Ras Samia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!