Monday , 26 February 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Urais wa Mnangagwa wapingwa mahakamani
Kimataifa

Urais wa Mnangagwa wapingwa mahakamani

Spread the love

CHAMA kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe ‘Movement for Democratic’ (MDC) kimeenda mahakamani kwa lengo la kukata rufaa, ili kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

MDC imeenda mahakamani ikidai kwamba kulifanyika udanganyifu katika matokeo ya urais yaliyompa ushindi Rais Emmerson Mnangagwa.

Kiongozi wa MDC, Nelson Chamisa amesema timu ya mawakili imefanikiwa kuwasilisha nyaraka za kesi hiyo katika mahakama ya kikatiba.

Chamisa amesema madai yao makuu ni mahakama imtangaze mshindi wa uchaguzi wa rais au iitishe ushaguzi mpya.

Hatua hiyo inakuja baada ya Chamisa kupoteza ushindi kwa kura chache kwenye uchaguzi wa Julai 30 dhidi ya rais wa sasa Emmerson Mnangagwa.

Matokeo ya tume ya uchaguzi yalionyesha kuwa Mnangagwa alipata asilimia 50.8 ya kura akifuatwa na Chamisa akiwa na asilimia 44.3. Lakini Chamisa anadai alipata asilimia 56 ya kura.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wanajeshi Ukraine waishiwa risasi, 31,000 wauawa

Spread the loveRais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy amesema zaidi ya wanajeshi 31,000...

Kimataifa

Waziri mkuu Palestina ajiuzulu

Spread the loveWaziri Mkuu wa Palestina, Mohammed Shtayyeh ametangaza kujiuzulu pamoja na...

Kimataifa

Rais mstaafu ahukumiwa miaka 4 jela

Spread the loveMahakama ya mjini Tunis imemhukumu rais wa zamani wa Tunisia,...

Kimataifa

Malawi yaondoa vikwazo vya viza kwa nchi 79 ikiwamo TZ

Spread the loveWaziri wa usalama wa ndani nchini Malawi, Ken Zikhałe ametangaza...

error: Content is protected !!