Friday , 2 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa NEC watoa neno kwa wagombea, wapiga kura
Habari za SiasaTangulizi

NEC watoa neno kwa wagombea, wapiga kura

Spread the love

IKIWA kesho tarehe 12 Agosti, 2018 ni siku ya upigaji kura katika uchaguzi mdogo wa ubunge Buyungu na kata thelathini na sita (36), Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa neno kwa wapiga kura. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage amewataka wagombea katika uchaguzi huo pale panapokuwa na malalamiko yoyote ya ukiukwaji wa Sheria na Taratibu za Uchaguzi, wayafikishwe kwenye mamlaka inayohusika kwa utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa Sheria.

Hali kadhalika, amewataka wagombea na wafuasi wao na wananchi kwa ujumla wajiepushe na vitendo vinavyoweza kusababisha fujo au vurugu katika vituo vya Kupigia, Kuhesabia na Kujumlishia Kura.

Akielezea kuhusu taratibu za upigaji kura hapo kesho, Jaji Kaijage amesemaUpigaji kura utafanyika katika vituo vile vile vilivyotumika wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na vitafunguliwa saa moja kamili  asubuhi na kufungwa saa kumi kamili jioni.

Na kwamba Iwapo, wakati wa kufunga kituo watakuwepo wapiga kura katika mstari ambao wamefika kabla ya saa kumi jioni na hawajapiga kura, wataruhusiwa kupiga kura. Isipokuwa wale watakaokuja baada ya muda huo hawataruhusiwa kujiunga katika mstari wa wapiga kura.

Vile vile, amesema watakaoruhusiwa kupiga kura ni wale tu ambao wamo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwenye Jimbo au Kata husika, na wana kadi ya mpiga kura. Hata hivyo, Tume kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 61(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, pamoja na kifungu cha 62(1) cha Sheria  ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, imeruhusu wapiga kura ambao ama kwa bahati mbaya wamepoteza kadi zao za kupigia kura au zimeharibika au zimechakaa watumie mojawapo ya vitambulisho vifuatavyo, Pasi ya Kusafiria, Leseni ya Udereva au Kitambulisho cha Uraia kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Pia, amesema mpiga kura aliyepoteza kadi yake ya kupigia kura au kadi hiyo kuharibika au kuchakaa ataweza kuruhusiwa kutumia Vitambulisho hivyo mbadala, iwapo tu; atakuwa aliandikishwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mwaka 2015, jina lake liwe katika orodha ya Wapiga Kura katika kituo anachokwenda kupiga Kura na majina yake yaliyopo katika Daftari la Mpiga Kura yafanane kwa herufi, maneno na tarakimu na majina yaliyopo katika kitambulisho mbadala.

Katika hatua nyingine, Jaji Kaijage amevipongeza Vyama vya Siasa vilivyojitokeza kushiriki uchaguzi huo mdogo kwa kuwadhamini Wagombea waliochukuwa fomu na hatimaye kuteuliwa kuwania nafasi hizo zilizo wazi za Ubunge na Udiwani.

“Nitumie nafasi hii pia kuwapongeza wananchi wote katika Jimbo la Buyungu na Kata Thelathini na Sita (36) zinazohusika na uchaguzi huu, kwa utulivu mliouonyesha wakati wote wa kipindi cha Kampeni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Bosi NIC apandishwa kizimbani, akabiliwa na mashitaka 365

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa...

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

Habari za SiasaTangulizi

Zanzibar watangaza rasmi kuwa shamba la Razaba ni mali yao

Spread the love  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...

error: Content is protected !!