Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Upinzani kuchukua nchi Malawi
Kimataifa

Upinzani kuchukua nchi Malawi

Spread the love

KUNA kila dalili kwamba, mgombea wa upinzani nchini Malawi, anaweza kutangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais uliofanyika juzi tarehe 23 Juni 2020. Unaripoti mtandao wa Nyasatimes…(endelea).

Taarifa za awali kwenye zoezi la kuhesabu kura zinaonesha, kiongozi wa upinzani Lazarus Chakwera (MCP), anaongoza kwa zaidi ya asilimia 60 wakati Peter Mutharika (DPP), rais anayetetea kiti chake akiwa na asilimia 38.

Kituo kinachotumika kukusanya taarifa za matokeo ya uchaguzi huo katika kila eneo nchini humo ‘Tonse Alliance Tally Centre,’ kimeeleza mpaka sasa Chakwera anaongoza kwenye matokeo hao.

“Mpaka sasa namba zinaonesha Chakwera mwenye miaka 65 amepata kura 2 373 317 sawa na asilimia 61.3 dhidi ya Mutharika (79) ambaye amepata kura 1 472 108 sawa na asilimia 38.01. mgombea wa tati Mbakuwaku amepata kura 27 821 sawa na silimia 0.72,” kimeeleza kituo hicho.

Licha ya taarifa hiyo, Tume ya Uchaguzi ya Malawi (MEC) imeeleza kuwa na asilimia 5 ta matokeo yote ya nchini.

Pia serikali imewataka wananchi, wanachama na wanasiasa kutochapisha taaifa za kupika kuhusu uchaguzi huo kwenye mitandao ya kijamii kwamba, hatua hiyo inaweza kusabaisha matatizo.

“Katika mazingira haya, wananchi wanaweza kuamini taarifa za kweli kwa sababu watakuwa wakilinganisha na taarifa za matokeo kutoka MEC,” imeeleza taarifa iliyotolewa na serikali.

Kwa maelezo ya tume ya uchaguzi, raia wa Malawi wanaofikia milioni 6.8, ndio walio na haki ya kupiga kura ambapo vituo vya kupigia kura zaidi ya 5,000 vimefunguliwa katika taifa hilo lililo na jumla ya watu milioni 17.5.

Uchaguzi huo unafanyika ikiwa ni baada ya miezi mitano kwa Mahakama ya Katiba nchini humo, kufuta matokeo ya uchaguzi wa mwaka jana uliobainika kuwa na kasoro ikiwemo kuiba kura.

Kwenye uchaguzi huo wa Mei 2019, Tume ya Uchaguzi nchini humo ilimtangaza Peter Mutharika kushinda kwa asilimia 38.5. Kwa mujibu wa sheria mpya ya uchaguzi nchini humo, mshindi sasa atahitaji kupata asilimia 51 ya kura zote.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!