September 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba kutangazia ubingwa Mbeya

Spread the love

TIMU ya Simba inahitaji pointi mbili kutangaza ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya tatu mfululizo baada ya jana kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Simba sasa inajumla ya pointi 78, ikifuiatiwa na Azam yenye pointi 58, huku nafasi ya tatu ikishikwa na Yanga yenye pointi 57.

Kama Simba itashinda kwenye mchezo wake dhidi ya Tanzania Prisons, mwisho wa juma hili itafikisha jumla ya pointi 81, ambayo haitaweza kufikiwa timu yoyote hata wakishinda kwenye michezo yao saba iliyosalia.

Azam FC ambayo inashika nafasi ya pili yenye pointi 58, ikifanikiwa kushinda michezo yake saba iliyosalia itakuwa na pointi 79.

Katika michezo 31 iiyocheza Simba, imeshinda mechi 25, imetoka sare michezo mitatu na kufungwa mechi tatu huku ikifunga jumla ya mabao 69 na kuruhusu mabao 16.

Urahisi wa Simba kutangza ubingwa kwenye mchezo ujao ulikuja mara baada ya Azam Fc, kupoteza mchezo wake mbele ya Kagera Sugar kwa bao 1-0, na Yanga kwenda sare ya Mabao 2-2 dhidi ya Namungo FC.

Mpaka sasa klabu zote zimecheza michezo 31, na kusalia mechi saba tu ili msimu uweze kumalizika na timu itakayoshika nafasi ya kwanza itaiwakilisha nchi kwenye michuano ya klabu bingwa barani Afrika.

Ligi hiyo itaendelea tena mwisho wa juma hili kwa kuchezwa michezo 10, kwa siku za Jumamosi na Jumapili.

error: Content is protected !!