Saturday , 9 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Waziri Mkuu Majaliwa awaondoa hofu wakulima Tanzania
Habari za Siasa

Waziri Mkuu Majaliwa awaondoa hofu wakulima Tanzania

Spread the love

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, amewataka wakulima wa mazao mbalimbali ya biashara wakiwemo wakulima wa ufuta waendelee na kilimo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Ruangwa … (endelea).

Majaliwa amesema suala la kushuka kwa bei lililotokea kwenye msimu wa mwaka huu lisiwakatishe tamaa kwani jambo hilo litakwisha.

Amesema Serikali inaendelea kulifanyia kazi hilo na bei ya mazao nchini itaimarika baada ya kuongezeka kwa ujenzi wa viwanda vya kuchakata mazao nchini, ambapo wakulima watakuwa na masoko na uhakika na pia nchi itauza bidhaa zitokanazo na mazao hayo na si malighafi.

Taarifa iliyotumwa kwa umma na Ofisi ya Waziri Mkuu imesema, Majaliwa alitoa kauli hiyo jana jioni Jumatano tarehe 24 Juni  2020 wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kata ya Nachingwea wilayani Ruangwa, Lindi alipokuwa katika ziara ya kikazina aliwasihi wakulima kutoacha kulima.

“Kushuka kwa bei ya ufuta kusiwakatishe tamaa na kuwafanya muache kulima kwa sababu bei haijashuka kwa zao hilo tu bali na mazao mengine kama chai, tumbaku, kahawa, chai na mazao mengine. Hali hii imetokana na mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 ambao umeikumba dunia.”

Ufuta ukiwa umekauka

Waziri mkuu alisema Serikali inatarajia kwamba kadiri ugonjwa wa COVID-19 unavyoendelea kupungua katika Mataifa mbalimbali duniani hali bei ya mazao nayo itaimarika, hivyo wakulima waendelee kuwa na subira katika kipindi hiki ambacho ni cha mpito.

Majaliwa ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa alitumia fursa hiyo kuwaalika wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi waje wawekeze katika viwanda vya kuchakata mazao mbalimbali kwa sababu watakuwa na uhakika wa upatikanaji wa malighafi pamoja na nishati ya kutosha.

Alisema moja ya msisitizo wa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli ni kuboresha sekta ya kilimo ili iweze kujitosheleza kwa chakula. “Suala la bei ya mazao linapangwa na wanunuzi Serikali inasimamia tu.”

Pia, waziri mkuu ameendelea kuwashukuru wananchi wa wilaya hiyo kwa umoja na mshikamano mkubwa waliompatia katika kipindi chote cha miaka mitano na amewasisitiza waendelee na ushirikiano huo kwa ajili ya maendeleo ya wilaya yao na Taifa kwa ujumla.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Miaka 62 ya uhuru tujenge upya mioyo yetu

Spread the loveWAKATI Tanganyika ikiadhimisha miaka 62 tangu kupata uhuru, Mwenyekiti wa...

Habari za Siasa

Rais Samia asamehe wafungwa 2,244

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewasamehe wafungwa 2,244, huku akiwabadilishia...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataka jamii inayohoji mafisadi

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan ametoa maagizo juu ya uboreshaji dira...

Habari za SiasaTangulizi

Kapinga: Kukatika kwa umeme siyo hujuma

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema Serikali ipo kazini...

error: Content is protected !!