September 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

UN: video ya ngono yasimamisha kazi wawili

UN logo

Spread the love

MAOFISA wawili wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN), waliokuwa wanaotajwa kufanya ngono kwenye gari la shirika hilo nchini Israel, wamepelekwa likizo ya bila malipo. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Wafanyakazi hao wawili, walipigwa picha ya video wakiwa kwenye gari lenye nembo ya UN katika mji wa Tel Aviv, Mtaa wa Ufukweni wakiwa wanafanya kitendo hicho.

Kwenye video hiyo iliyowekwa mtandaoni na kuripotiwa pakubwa duniani, mwanamke aliyekuwa amevaa gauni jekundu, alimkalia mwanamue nyuma ya dereva huku wakifanya kitendo hicho.

Mtu mmoja mtaani hapo, akiwa kwa juu kidogo alifanikiwa kupiga picha hiyo. Alifanikiwa kufanya hivyo wakati gari hilo likiwa kwenye taa za barabarani likisubiri kuondoka.

Sekunde chache baadaye, taa ziliruhusu kuondoka na gari hilo liliondoka huku ‘shughuli’ ikiwa inaendelea nyuma ya kiti cha dereva,

Ilikuwa rahisi kuonekana kwa watu hao wakifanya ‘mambo’ kwa kuwa, gari hilo vioo vyake havikuwekwa giza ‘tinted.’

Stéphane Dujarric, Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja UN alitaja kitendo hicho kwamba ni cha kuchukiza na kushtua.

Mpaka sasa, UN imebaini kuwa wanahusika hao ni waajiriwa katika taasisi yake ya Kusimamia Kusitishwa kwa Mapigano (UNTSO).

error: Content is protected !!