Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Ukraine wadai kuua wanajeshi 5,840 wa Urusi
Kimataifa

Ukraine wadai kuua wanajeshi 5,840 wa Urusi

Spread the love

 

JESHI la Ukraine limedai kuua wanajeshi 5,840 wa Urusi tangu kuanza kwa vita kati ya nchi hizo mbili siku saba zilizopita. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 2 Machi, 2022 na Kamanda Mkuu wa Jeshi la Ukraine, Valeriy Zaluzhny kwa vyombo vya habari wakati akitoa takwimu mbalimbali za vita hiyo.

Kwa mujibu wa BBC, jumla ya hasara ambayo Ukraine imedai Urusi imepata katika vita hiyo ni pamoja na kupoteza wanajeshi 5,840, ndege 30, helkopta 31 na vifaru 211.

Pia Urusi imepoteza magari ya doria 862, vifaru vya 85 vyenye mfumo wa kutungua ndege, makombora 9, matenki 69 ya mafuta, magari 355 na mitambo 40 ya kurusha roketi.

Hata hivyo, madai hayajathibitishwa licha ya Waziri wa Ulinzi wa Uingereza, Ben Wallace kusema anaamini Majeshi ya Putin yamepata hasara kubwa wakati wa uvamizi wa Ukraine.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!