October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Urusi waendelea kuteka miji muhimu Ukraine

Spread the love

 

Vikosi vya Jeshi la Urusi vimeendelea kusonga mbele katika kushambulia na kuteka miji muhimu nchini Ukraine ambapo wanadai kuuteta mji wa Kherson ambao ndio wenye bandari kubwa nchini humo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Meya wa jimbo hilo hilo lililopo kusini mwa Ukraine, Igor Kolykhayev amesema wamezingirwa lakini wamekanusha kutekwa kwa mji huo na majeshi ya Urusi.

Kutekwa kwa mji huo kunaonekana kuwa na umuhimu na msaada mkubwa kwa Urusi kutokana na kuwa katika eneo la kimkakati linalotumika na Ukraine kuingiza bidhaa ambapo Urusi itaidhibiti Ukraine na yenyewe kuutumia kuingiza vifaa na majeshi yake.

Pia majeshi ya Urusi yanaripotiwa pia kuuteka mji wa Kharkiv uliopo Kaskazini Mashariki mwa Ukraine ambapo wanaripotiwa kulipua jengo moja la Ofisi ya Jeshi la Polisi na Usalama wa Ukraine.

Watu wanne wanaripotiwa kufariki katika shambulizi hilo asubuhi ya kuamkia leo tarehe 2 Machi, 2022.

error: Content is protected !!