Tuesday , 18 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ujerumani kuwalipa fidia wahanga wa ukoloni Tanzania, kurejesha mabaki
Habari za SiasaTangulizi

Ujerumani kuwalipa fidia wahanga wa ukoloni Tanzania, kurejesha mabaki

Spread the love

RAIS wa Shirikisho la Ujerumani, Dk. Frank Walter Steinmeier, ameahidi kufanya mazungumzo na watu walioathiriwa na ukoloni uliofanywa na taifa hilo, juu ya namna ya kuwafuta machozi, pamoja na kurejesha mabaki ya miili ya watu yaliyohifadhiwa katika makumbusho ya nchini kwao. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Rais Steinmeier ametoa ahadi hiyo leo tarehe 31 Oktoba 2023, Ikulu jijini Dar es Salaam, katika mkutano ulioandaliwa kwa ajili ya kutoa mrejesho wa masuala waliyojadili na kuafikiana na Rais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan.

“Tuweze kuangalia ukurasa mpya, ziara hii pia nimeiweka katika mrengo wa kuangalia yaliyotokea wakati wa ukoloni na kuonana na walioathiriwa na vita ya majimaji na pia nitakwenda kukutana na baadhi ya wahanga na nitaongea nao sababu najua walipitia kipindi kigumu. Yote watakayonieleza nitakwenda kuyarudisha Ujerumani,” amesema Rais Steinmeier.

Aidha, kiongozi huyo wa Ujerumani, amesema watafanya utafiti ili kujua athari zilizotokana na ukoloni.

“Tumejadiliana kuhusu namna gani ushirikiano uliopo utaweza kuendelezwa na tusisahau yaliyopita kati ya Ujerumani na Tanzania, kuna mambo tumepitia wakati wa ukoloni ni muhimu tuweze kukubaliana na tumefikia maamuzi kufanya utafiti wa ndani tuweze kuongeza maarifa katika hiki kilichotokea wakati wa ukoloni,” amesema Rais Steinmeier.

Awali, Rais Samia alisema katika mazungumzo yake na Rais Steinmeier, wamekubaliana kufungua majadiliano kuona jinsi ya kuzifuta machozi familia zilizoathiriwa wakati ilipokuwa inatawala Tanganyika.

“Kama mnavyojua Tanzania wakati ule Tanganyika, nadhani hata Zanzibar kwa muda mdogo tulikuwa chini ya utawala wa Ujerumani. Sasa katika utawala mambo mengi yamepita nimezungumza kwa urefu na tuko tayari kufungua majadiliano na kuona jinsi tutakavyoweza kukubaliana kwa yale yaliyopita Wakati wa utawala wa Ujerumani,” alisema Rais Samia na kuongeza:

“Vipi tufanye na najua kuna familia ambazo zinasubiri mabaki ya wapendwa wao ambayo yako kule makumbusho yaje yote. Tunakwenda kuzungumza na kuona vipi twende nayo vizuri.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mazingira magumu ya JPM yamechangia ‘Comedy Journalism’

Spread the loveMwenyekiti wa Kamati ya kufuatilia hali ya uchumi wa vyombo...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

RC Chalamila: Nimeacha ubabe

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chamalila amemthibishia...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia atoa ujumbe mzito Sikukuu Eid Al Adha

Spread the loveKATIKA kusherehekea Sikukuu ya Eid Al Adha, Rais wa Tanzania,...

BiasharaHabari za Siasa

Dk. Biteko aipongeza NMB kwa kuanzisha utoaji wa bima ya mifugo

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!